Saturday 23 June 2018

UHUSIANO KATI YA ROHO NA MATUMIZI YA AKILI.

BWANA YESU ASIFIWE

Namshukuru sana Mungu kwa kuwa amekusudia tena huu uwe wakati mzuri sana wa kujifunza tena neno lake kwaajili ya utukufu wake
Siyo hali ya kawaida wala rahisi sana bali ni kwa neema zake na fadhili zake tu ambazo kwetu hazikomi.
Leo tunajifunza somo lenye kichwa kinachosema,

UHUSIANO KATI YA ROHO NA MATUMIZI YA AKILI.

Ndugu yangu katika Kristo Yesu, Mungu alimpa mwanadamu kila kitu kwa kusudi lake ili kuyatatua mambo mbalimbali anayoweza kukutana nayo katika maisha yake.
Ila katika kukuwekea hivyo vitu bado unatakiwa umtegemee yeye.
Yupo Mungu anayetusaidia katika changamoto zote tunazokutana nazo lakini anatusaidia kupitia vitu alivyoviweka ndani yetu ambavyo siyo vya bure tunapaswa kuvitumia huku tukimtegemea yeye kuviwezesha zaidi katika utendaji maana pia anasema katika neno lake kwamba sisi hatuwezi kufanya neno lolote bila yeye.
BWANA YESU ASIFIWE.

Kati ya vitu vingi Mungu alivyoviweka ndani yetu kama macho, miguu, mikono, nguvu n.k,
Leo amekusudia tujifunze namna ya kutumia akili zetu.

ISAYA 11:2
Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;

*******************

Huyu ni Mungu alimwekea mwanadamu vitu vyote hivi ili vimsaidie katika utendaji wake na vitu anavyovitumia ili kufanikisha kila anachokusudia kifanyike.
Usipotumia hata kimoja kati ya hivi ni lazima utaona mapungufu makubwa sana katika maisha yako.

Ipo Roho ya Bwana ambayo ni ya wewe kutambua uwepo wa Mungu katika maisha yako na katika njia zako zote.
Ipo Roho ya HEKIMA
Roho ya UFAHAMU
Roho ya SHAURI
Roho ya UWEZA
Roho ya MAARIFA
Na Roho ya kumcha BWANA.

Hivi vyote tunapaswa kuvitumia maana vipo ndani yetu kwa uwezo wa Roho mtakatifu ambaye alipewa jukumu la kulisaidia kanisa ambapo kanisa ni mimi na wewe tulio ndani ya Kristo.

YOHANA 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

****************

Roho Mtakatifu anatufundisha ili tuwe na akili itakayoweza kuchangunyua mambo na tuweze kufikiri kwa kina namna ya kuweza kutoka kwenye matatizo mbalimbali.

Hizi akili Mungu aliziweka ndani yetu ili tuweze kuzitumia tupate mafanikio.

ISAYA 48:17
BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

*******************

Mungu anasema anakufundisha ili upate faida.
Lakini anapokufundisha kabla hujapata faida huwa unapata akili kwanza ambayo itakuwezesha wewe kufikiri na kupata majibu kwamba utapataje faida.
Anasema anakuongoza njia ikupasayo kuifuata.
Unapokuwa unamuomba Mungu yeye atakujibu kwa kukuongoza njia, sasa unatakiwa uifuate.

MWANZO 41:33
Basi, Farao na ajitafutie mtu wa akili na hekima amweke juu ya nchi ya Misri.

********************

Wakati Mungu alipomtaarifu Farao juu ya njaa itakayotokea katika nchi ya Misri Mungu alimwambia atafute mtu mwenye akili na hekima akijuwa kabisa bila akili kutumika pale hakuna kitakacholeta matokeo mazuri.
Mungu alishafanya kwa sehemu yake iliyopita fahamu na akili ambayo ni kumjulisha, sasa kilichobaki ni akili kutumika ili Farao ajue afanyeje katika miaka ya mwanzo ya shibe ili miaka itakayofuata ya njaa apate faida.

MWANZO 41:38-40
Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?

Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.

Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe.

*****************

Pia Farao alipoona inastahili mtu mwenye akili bado akaona kuna haja ya Mungu kutegemewa katika hizo akili zitakazotumika.

Akagundua kuwa huyohuyo Mungu aliyemtumia kuyasema hayo atakuwa ana Mungu ndani yake.

Farao akamweka kuwa juu kuliko watu wote katika Misri isipokuwa yeye Farao tu!
Ni kwasababu Yusufu alikuwa mcha Mungu na na aliyetumia akili ndiyo maana akawa juu kiasi kile.

Angekuwa mcha Mungu peke yake isingetosha na wala angekuwa mwenye akili peke yake isingetosha na ndiyo maana Farao alisema
(Tupate wapi MTU mwenye akili na Roho ya Mungu ndani yake?)

METHALI 3:5-6
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Katika njia zako zote mkiri yeye,Naye atayanyosha mapito yako.

**************

Tunatakiwa kumtumainia Mungu na tumkiri kwamba yeye anaweza katika njia zetu lakini tutumie akile huku tukimtegemea yeye.

Unapotumia akili hapo unakuwa umeshamtegemea maana umeheshimu kile alichokiweka ndani yako.

METHALI 1:29-32
Kwa kuwa walichukia maarifa,Wala hawakuchagua kumcha BWANA.

Hawakukubali mashauri yangu,Wakayadharau maonyo yangu yote.

Kwa hiyo watakula matunda ya njia yao,Watashiba mashauri yao wenyewe.

Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua,Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza.

***************
Mungu anasema hawa watu walichukia maarifa yake wakapenda ya kwao wala hawakutaka kumcha BWANA.
Waliwaza kibinadamu wakaenda kwa nguvu zao wenyewe.

Wakadharau kila Mungu alichowaelekeza.
Mungu anasema watakula matunda ya njia zao na kushiba mashauri yao.

Inamaana upo uwezekano wa mtu kutokutambua uwepo wa Mungu wala asitake kabisa kumtegemea wala kufikiri kwa akili ya Kiungu na akashiba kwa shauri lake mwenyewe.

Wapumbavu ni wale waliolikataa neno la Mungu maana hata biblia inasema mpumbavu husema moyoni mwake kwamba hakuna Mungu.

Sasa huyu huyu anayesema moyoni mwake kwamba hakuna Mungu huwa anafanikiwa lakini Mungu anasema kufanikiwa kwake kutamwangamiza.

Ataangamia kwasababu kila atakachowaza na matokeo ya mawazo yake hayatatokana na Mungu.

ISAYA 55:8
Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA.

*****************

Mungu anaendelea kutofautisha mawazo yake na mawazo ya mwanadamu.
Huwa akili ndiyo inayotumika kuwaza na Mungu anasema kuwa katika utendaji na maamuzi yake huwa anatumia akili kuwaza.
Na mawazo anayowaza yeye hayalingani na mawazo yetu hata kidogo.

MATHAYO 22:36-38
Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu?

Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza.

****************

Mungu pia anataka tutumie akili zetu zote kumpenda yeye.
Na usipompenda Mungu kwa akili ukampenda kwa Roho tu ni lazima utaangamia.

Ukimpenda Mungu kwa Roho tu utajikuta kuna sehemu unatakiwa kabisa utumie akili lakini unaishia kukemea kwa jina la Yesu huku ukiangamia.
Kwa akili za kawaida unamuona nyoka kaingia ndani wewe unakemea kwa jina la Yesu eti afe bila kumpiga.
Unatakiwa ukemee huku unampiga, kanuni ya kitu chochote kinachoishi ili kife ni lazima kitolewe uhai hiyo ndiyo akili.

Mungu pale atakusaidia tu asikudhuru lakini kumpiga ni jukumu lako na ujue hapo umekosa maarifa maana vita vyetu ni katika ulimwengu wa Roho.
Hata Yesu kuna siku walikuwa wanataka kumpiga na mawe lakini akakimbia na kujificha.
Alikuwa mwenye nguvu za kuwafanya chochote lakini pale alikuwa anatutengenezea kanuni kwamba hata ukiwa umeokoka na Yesu yuko ndani yako bado unatakiwa utumie akili na uangalie nyakati maana biblia inasema alikimbia kwamaana saa yake ya kupigwa ilikuwa haijawadia.

Hivyo usipotumia akili yako sawasawa kuna uwezekano wa kuishi maisha ambayo hukupaswa kuishi kwa wakati uliopo.

2WAKORINTHO 4:4
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

****************

Mungu amempa shetani jina mungu wa dunia hii kwa jinsi anavyocheza na akili za watu.
Shetani huwa hatumii nguvu bali anacheza tu na ufahamu wako.
Anajuwa kabisa akishapofusha fikra zako basi na akili zitalala na hutamjuwa Mungu maana pasipo akili hutaweza kumpenda Mungu.
Kumbuka Mungu amesema umpende kwa akili zako zote.

Sasa anapofusha fikra zako zisiweze kuona mbele na akili inalala.

Hivyo sifa ya kwanza kwa mtu ambye hajaokoka na kumpenda Mungu ni kwamba Hana akili na fikra zake zimepofushwa.

Nuru ya injili haiko kwake  hivyo hata ukimhubiria hatakuelewa kwasababu hana akili ya kutafakari neno ili Roho alihuishe ndani yake.
Hata ukitaka kumwombea mtu huyu unatakiwa uombee akili zake.
Utasikia anamtaja taja Yesu Yesu lakini hana akili za kuchambua ajue Yesu anapatikanaje ila yeye ana ujinga ndani yake wa kujaribu tu kupingana na akili za Mungu.

LUKA 24:45
Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko.

**************
Kumbe akili zisipotumika sawasawa huwezi ukayaelewa maandiko.
Ili ujue nguvu ya akili ilivyo angalia hapa.

Kumbuka Yesu alipokuwa akiondoka kwenda mbinguni alisema atamtuma kwetu huyo Roho mtakatifu ili atufundishe na kutukumbusha.
Na huyo Roho alikuwa ndani yake pia.
Inamaana bila huyo Roho hatuwezi kuelewa wala kukumbuka.

Na hapa alipowafunulia akili zao alikuwa hajaondoka bado, kwahiyo Roho hakuwa ndani yao.
Lakini walipofunuliwa akili zao wakaelewa maandiko.
Hivyo yeye aliweza kwakuwa huyo Roho alikuwa ndani yake, lakini pasipo akili hawakuelewa.

HESABU 13:30-33
Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka.

Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi.

Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.

Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.

**************

Hapa walikuwa watu 12 walioenda kuipeleleza nchi na wote walikuwa pamoja safari nzima.
Hakuna aliyeona vitu tofauti na mwingine lakini kati yao wawili tu waliona tofauti japokuwa vitu walivyoviona vilikuwa sawa.

Kalebu anasema tunaweza kushinda lakini wengine wanasema hatuwezi kwa kwawa waliwakuta watu kule wakajiona nafsi zao kama mapanzi.

Hao watu waliowakuta kule hawakuwaambia kuwa nyie ni mapanzi lakini wao wenyewe walijiona mapanzi na walipojiona mapanzi wakaonekana mapanzi kweli.

METHALI 23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.Akuambia, Haya, kula, kunywa;Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.

******************
Unajuwa ni kwanini hawa watu walileta majibu tofauti?

Wale kumi walioleta habari mbaya walitazama kiakili tu hawakutazama kiroho.

Wale wawili walitazama kiroho na kiakili pia.
Waliwaona ni warefu kweli kiakili lakini kiroho wakaonekana si kitu.

WAEBRANIA 4:2
Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.

***************
Wote walimsikia Mungu namna alivyowaambia kwamba atawashindia lakini wapo waliosikia tu bila imani ndiyo wale kumi pamoja na waliozipokea habari zao.

Hapo ndipo walipotumia akili lakini hawakuzitegemea wakamtegemea Mungu.

Kwa kuwa sasa hao wengine kumi hawakutumia akili zao pamoja na kumsikiliza Mungu hivyo hawakuirithi ile nchi.
Wote walifia jangwani kwasababu ya kutokuhusisha akili na Roho.

AKILI NI LAZIMA ZITUMIKE ILI KUFIKIA MAFANIKIO.

KUTOKA 18:19-23
Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;

nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonyesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya.

Zaidi ya hayo utajipatia katika watu hawa watu walio na uwezo, wenye kumcha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukia mapato ya udhalimu; ukawaweka juu yao, wawe wakuu wa maelfu, na wakuu wa mia, na wakuu wa hamsini, na wakuu wa kumi;

nao wawaamue watu hawa sikuzote; kisha, kila neno lililo kubwa watakuletea wewe, lakini kila neno dogo wataliamua wenyewe; basi kwako wewe mwenyewe utapata nafasi zaidi, nao watauchukua huo mzigo pamoja nawe.

Kwamba utafanya jambo hili, na Mungu akikuagiza hivyo, basi utaweza kusimama wewe, na watu hawa wote nao watakwenda mahali pao kwa amani.

***************
Huyu ni Yethro mkwewe Musa alikuwa anamshauri Musa baada ya kuona wana wa Israeli wanamwendea mmoja mmoja ili awafundishe pamoja na kutatua matatizo yao.
Kwa jinsi walivyokuwa wengi Musa alizidiwa.

Musa ni mtu wa Mungu kabisa lakini hapa kuna akili hakuitumia ndiyo maana anapewa ushauri na ulimsaidia.

Ni akili ilitumika na ndiyo maana hata leo hii tunakuwa na mwakilishi mmoja tu bungeni hatuendi wote.

Ndiyo maana kuna wawakilishi wa Raisi ambao ni wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya na mawaziri.
Hizo zote ni Kazi za Raisi lakini ni akili ilitumika ili maendeleo ya nchi yaende haraka.
Pasipokutumia akili utajikuta unakwama na jambo ambalo ulitakiwa ulimalize leo utalimaliza mwakani.

Hizi mashine zinazotusaidia kurahisisha kazi tusingekuwa nazo bila kutumia akili na Mungu akatuwezesha.

Sasa kama huyu Musa asingepata ushauri huu asingeweza kabisa kutatua matatizo yote ya wana wa Israeli kwakuwa walikuwa wengi mno na matokeo yake wangeanza kumlaumu kwamba anawanyanyasa huko jangwani.

METHALI 28:16
Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.

****************

Ukiwa mkuu halafu ukapungukiwa tu na akili ni lazima watu wanyanyasike.
Unaweza ukawa Raisi au kiongozi ofisini na unatamani sana wananchi wako wewe Raisi au wafanyakazi wako wewe kiongozi waishi maisha mazuri lakini tatizo umepungukiwa na akili.

Huyu Musa alikuwa anatamani sana kutatua haraka haraka matatizo yote ya wana wa Israeli lakini hakuwa amepata hiyo akili ya kuwapanga watu kwa namna ile.

Angejikuta anatatua matatizo ya watu siku zote huko jangwani bila mafanikio.
Hivyo hata ukiona kiongozi wako anakuletea hali ya kukuonea wewe ombea akili zake.
Hata kama ni baba katika familia anawaonea mke na watoto wewe ombea akili zake maana zimepungua.
Huwa hapendi awaonee ila hana akili za kutosha kuwaridhisha.
Familia inahitaji akili kuiongoza na baba anapokosa akili tu kila kitu kinaharibika maana yeye ni kichwa.

1PETRO 3:7
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

*****************

Hasa sisi tulio okoka hapa panatakiwa akili kwelikweli.
Mimi mwanaume natakiwa kumwombea mke wangu.
Sasa nitaombaje kama akili yangu haijanionyesha cha kuombea?
Wewe unapaswa kumwombea lakini utumie akili kukaa nae.
Hujaambiwa ukae na mke kiroho tu bali na akili pia.
Wewe huwezi ukaangalia tu mke anarudi nyumbani na vitu fulani vya garama usizozijuwa au anachelewa kurudi halafu unajipa moyo tu kwamba ameokoka.

Wewe unamwomba Mungu akupe mke mwema halafu unakuta mwanamke unahisi umepewa na Mungu eti kisa ni mpendwa ameokoka na unakaa kirohoroho tu hutumii akili kumchunguza.

Mungu anapotaka umwombee mke/mume unatakiwa utumie akili kujuwa ni kipi natakiwa kuomba kwaajili yake.
Yapo ambayo hutayajuwa kwa akili zako na hapo ndopo Mungu huja na akili zake na uweza wake ili kuonyesha utukufu wake.

Unataka Mungu akuambie nini unapomuona mwanamke kavaa suruali na nguo ambazo unaona kabisa hazina nia nzuri?
HUNA AKILI YA KUTAFAKARI JUU YA HAYO MAVAZI?

Tumia akili na utafakari Mungu atakusaidia.
Upo muda wa kumfurahisha mke/mume kiakili na muda wa kumjenga kiroho pia.

Suala la kumfurahisha mwenzako kwenye ndoa na kumridhisha siyo la kiroho bali ni akili inatakiwa kutumika.

ZABURI 4:4
Mwe na hofu wala msitende dhambi,Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.

**************

Ili uwe na hofu na kutokutenda dhambi ni lazima utafakari ukitumia akili zako.

Akili yako itakuambia umsikilize Mungu naye Mungu ataipa akili yako uwezo wa kutafakari kwa akili ya Kiungu na utapata majibu yenye kibali mbele zake.

METHALI 24:30-34
Nalipita karibu na shamba la mvivu,Na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili.

Kumbe! Lote pia limemea miiba;Uso wake ulifunikwa kwa viwawi;Na ukuta wake wa mawe umebomoka.

Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana;Naliona, nikapata mafundisho.

Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,Bado kukunja mikono upate usingizi!

Hivyo, umaskini wako huja kama mnyanganyi,Na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha.

*****************

Angalia sasa shamba hili la mtu asiye na akili.
Ukikosa akili utapanda wala hutavuna.

Madhara ya mtu asiye na akili ni haya.

Umasikini huja kama mnyang'anyi.
Mnyang'anyi ni mtu anayekuja kukupokonya ulicho nacho wewe.
Ndivyo utakavyokuwa na mahitaji mengi bila msaada maana huna akili.

Mtu mwenye silaha huwezi kumzuia kukuvamia wewe.
Hivyo mahitaji yako muhimu yatakuja kwako kwa nguvu taka usitake kwakuwa huna akili.

Huyu mvivu anatajwa kwamba hana akili lakini hajatajwa kwamba hana Mungu.
Sasa huenda anaye Mungu lakini akili hana.
Huwezi ukawa mcha Mungu ukapanda halafu ukaomba Mungu shamba lijipalilie lenyewe.
Ni akili zako zitakuambia kwamba huu ni wakati wa kupalilia na huu ni wakati wa kuvuna na huu ni wakati wa kupanda au kukusanya ghalani.
Nyakati hizo zote zipo ili tuzitumie kulingana na jinsi zilivyo.
Huyu mtu mvivu asiye na akili ni lazima atakufa njaa kwaajili ya kutokutumia akili.

2WATHESOLONIKE 3:10
Kwa kuwa hata wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.

******************

Hapo Paulo anawaambia ikiwa mtu hataki kufanya kazi, basi, asile chakula.
Hajasema ikiwa mtu hataki kuokoka,
Hajasema ikiwa mtu hataki kumcha Mungu.

Na hiyo Kazi utaifanya kwa akili siyo kama huyo mvivu.
Muda wa kupalilia upalilie na muda wa kuweka dawa na mbolea ufanye hivyo.
Ukitumia akili yako sawasawa utashinda wala hutakuwa masikini.
TUMIA AKILI MTEGEMEE MUNGU.

ISAYA 40:28
Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.

*****************
Kumbuka kuna somo tulijifunza lenye kichwa kinachoitwa
THAMANI YA MWANADAMU (MTEULE)

Tuliona namna ambavyo sisi tumekuwa washirika wa tabia ya Mungu ya Uungu.
Mungu anasema akili zake hazichunguziki  na sisi ni washirika wa tabia yake na pia ni mfano wake.
Hivyo unapokuwa na Mungu akili zako hazitakuwa za kawaida na ndiyo maana sisi tuna uwezo ndani yetu wa kuzishinda hila zote za Yule mwovu.

2WAKORINTHO 10:5
tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

*****************

Kitu chochote kinachojiinua kuliko elimu ya Mungu aliyoiweka ndani yetu sisi tuna uwezo wa kukitiishi.

Kinachojiinua kinyume na elimu ni umbumbu, kujifanya wajuwaji zaidi, ujinga, na kutokutumia akili

Mungu anayo elimu na pia anatumia akili pia katika utendaji wake.

MWANZO 1:2
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

*****************

Roho ya Mungu ilitulia juu ya uso wa vilindi vya maji halafu neno likaanza kufanya kazi ndipo vyote vilivyoko duniani na viijazavyo vikatokea.

Lakini sasa katika uumbaji wa vyote kuna vitu ambavyo vilitumika.

AYUBU 38:33
Je! Unazijua amri zilizoamuriwa mbingu?Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?

****************

Kuna amri ambazo ziliamriwa ndipo mbingu zikawa kama zilivyo sasa.
Na hili swali ni Mungu alikuwa anamwuliza Ayubu siku za kujaribiwa kwake.
Alimwuliza akijuwa kabisa ni jambo ambalo Ayubu hawezi akalijuwa.
Lakini sasa tazama kilichotumika mpaka mbingu zikawa kama zilivyo.

METHALI 3:19-20
Kwa hekima BWANA aliiweka misingi ya nchi;Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;

Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika;Na mawingu yadondoza umande.

*****************

Kuwa makini hapa,
Roho ya Mungu ilipotulia juu ya vilindi vya maji alianza kutamka na neno likaumba.
Lakini hilo neno ambalo ni Yesu wakati anaumba alikuwa anatumia HEKIMA kuiweka misingi ya nchi,
Na kwa kutumia AKILI zake imara akazifanya mbingu imara.

Kwa MAARIFA yake vilindi viligawanyika.
Je kama Mungu alitumia akili japo ndiye mwenye nguvu wewe unatarajia uwe na nguvu za kiroho halafu usitumie akili ufanikiwe?
Wapo watu makanisani wanalijuwa neno, ni waombaji wazuri, wanatoa mapepo kwa jina la Yesu lakini akili za kupata maendelea hawana.
Lakini huo sio mpango wa Mungu ukue kiroho tu na uwe masikini.

3YOHANE 1:2
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

**************

Mungu anataka tufanikiwe katika mambo yote.
Kiroho, kimwili na kila aina ya mafanikio.
Katika sisi kufanikiwa tunatakiwa kutumia vitu mbalimbali Mungu alivyoviweka ndani yetu.

Mungu alikuwekea huo ubongo siyo mapambo bali utumie alichokiweka ndani yake.

Mwanadamu amepewa vitu vikubwa sana.
Pamoja na vitu mbalimbali na utandawazi unaouona hapa duniani bado mwanadamu hajatumia hata robo ya kiwango cha uwezo wa akili ambazo Mungu aliziweka ndani yake.
Hakuna hata mtu mmoja hapa duniani aliyetumia asilimia 50% kati ya asilimia 100% ya akili ambazo Mungu alizoziweka kwa wanadamu.

Ili uweze kutumia akili zako unatakiwa umwombe Mungu akufungue fahamu zako, roho ya umbumbumbu ikuachie upate maarifa na Mungu wetu ni mwaminifu utaweza kutumia akili zako ukapata mafanikio.

Na usiseme unazo akili, wewe bado huna akili.
Ukishafanya maombi maalumu ukaombea akili zako halafu zikafunguka ndipo utakapogunduwa kumbe hukuwa na akili.
Hakuna mjinga anayejijuwa kuwa yeye ni mjinga.
Bali waliomzidi akili ndiyo huwa wanamwona ni mjinga.
Hata huyo mjinga na ujinga wake wapo aliowazidi akili nao wanamwona ana akili.

Nenda mbele za Mungu ukiri kwamba wewe huna akili na umwombe akupe maarifa na akili akufundishe ili upate faida.

ASANTE SANA ROHO MTAKATIFU MAANA WEWE NI MWALIMU MWEMA UNIPAYE AKILI, UNIFUNDISHAYE ILI NIPATE FAIDA.

MUNGU AKUBARIKI SANA.
#Powered_By_Holly_Spirit

IN ENGLISH


THE LORD JESUS ​​IS NOT DONE

I thank God that he has purposed this again a wonderful time to learn his Word again for his glory
It's not normal nor easy but it's only by his grace and grace that we do not live.
Today we study a lesson with the theme,

RELATIONSHIP WITH THE HEART OF THE SPIRIT AND THE PERSONAL SERVICE.

My brother in Christ Jesus, God gave everything to humankind for his purpose in resolving a variety of things he might encounter in his life.
Besides putting you in so much stuff you still have to rely on him.
There is a God who helps us in all the challenges we face but helps us through what he has put in us that which is not free we should use as we rely on him to make it more practical in his own sense as he also says in his word that we can not do anything without him.
THE LORD JESUS ​​IS NOT DONE.

Among the many things God has put in us as eyes, feet, hands, strengths,
Today he has intended to learn how to use our mind.

ISAIAH 11: 2
And the Spirit of the LORD shall dwell upon him, the spirit of wisdom and understanding, the spirit of counsel and of mightiness, the spirit of knowledge and of the fear of the LORD;

*******************

This is God who has given humans all these things to help him in his work and resources to achieve whatever he purposes to do.
If you do not use one or more of these you will have to see the biggest shortcomings in your life.

Where the Spirit of the Lord is for you to recognize the presence of God in your life and in all your ways.
Where the Spirit of LOVE
THE SPIRIT OF KNOW
SPIRIT OF THE WITNESS
Eternal Spirit
SPIRIT OF INFORMATION
With a spirit of fear of the Lord.

All of us should use the meaning of it in the power of the Holy Spirit who was given the responsibility of helping the church where the church and I are in Christ.

JOHN 14:26
But the Helper, the Holy Spirit, whom the Father will send in my name, will teach them all, and remind you of all that I have told you.

****************

The Holy Spirit teaches us to have a mind that will be able to glean things and we can think deeply about how to overcome from various problems.

These thoughts God put in us so that we can use them to succeed.

ISAIAH 48:17
Thus says the Lord, your Redeemer, the Holy One of Israel; I am the LORD thy God, which teacheth thee for thy profit, and I guide thee in the way that thou shouldest follow.

*******************

God says he teaches you to benefit.
But when he teaches you before you get the advantage you get the first idea that will enable you to think and find answers to how you will get the benefits.
He says he guides you the way you should follow it.
When you ask God he will answer you by guiding you the way, now you have to follow it.

ACTS 41:33
So let Phar'aoh look for a man of understanding and wisdom to set him over the land of Egypt.

*******************

When God told Pharaoh about the famine that would happen in the land of Egypt, God told him to search for an intelligent and wise man who was completely ignorant when there would be no good results.
God has done in his consciousness and intelligence part which is to inform him, but what remains remains intelligent to use what Pharaoh should do in the early years of the shibe for the next years of hunger to benefit.

ACTS 41: 38-40
And Pharaoh said unto his servants, Where can we find such a man as this, in whom is the spirit of God?

And Pharaoh said unto Joseph, Because God hath made thee known all this, there is none wise and wise as thou art.

So you will be over my house, and by your word my people will be governed. Only in the throne will I be greater than you.

*****************

When Pharaoh saw fit, a wise man still saw the need for God to be relied on in the minds that would be used.

He realized that what God used to say would have God in him.

Phar'aoh shouted to be higher than all the people in Egypt except he only Pharaoh!
It was because Joseph was a goddess and that he used intelligence was why he was so high.

He would only be selfish and would not be intelligent alone and that's why Pharaoh said
(Where can we get the intelligent man and the Spirit of God in it?)

ACTS 3: 5-6
Trust in the LORD with all your heart, and do not lean on your own mind;

In all your ways acknowledge him, and He will stretch forth your steps.

**************

We should trust God and confess that he can in our ways but send us away while we trust in Him.

When you use the mind there you rely on it because you respect what he put in you.

METHOD 1: 29-32
Because they hated knowledge, neither did they choose to fear the LORD.

They did not accept my counsel, They despised all my warnings.

Therefore shall they eat of the fruit of their way, And shall enjoy their own counsel.

For their backsliding the foolish shall kill them, And their prosperity shall destroy them.

***************
God says these people hated his knowledge of their love for them and did not want to fear the Lord.
They thought the humanity went in their own strength.

They despised every God that directed them.
God says they will eat the fruit of their way and satisfy their advice.

It conveys the possibility of one's ignorance of the existence of God and does not seek to rely on Him nor to think of Divine Mind and to be content with His own counsel.

Fools are those who reject the word of God, even though the Bible says that the fool says in his heart that there is no God.

Now this one who says in his heart that there is no God is successful but God says that his prosperity will destroy him.

He will perish because everything he will think and the consequences of his thoughts will not come from God.

ISAIAH 55: 8
For my thoughts are not your thoughts, nor are your ways my ways; says the Lord.

*****************

God continues to distinguish his thoughts from man's thoughts.
It is intelligent that is used to appeal and God says that in his actions and decisions he uses intelligence to scream.
And the thoughts that he thinks he does not fit our minds at all.

MATTHEW 22: 36-38
Teacher, which commandment is the main commandment?

And he said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.

This is the main commandment, and it is the first.

****************

God also wants us to use all our mind to love Him.
And if you do not love God wisely, if you love Him in the Spirit, you only must perish.

If you love God in the Spirit only you will find that there is a place where you really need to use the mind but you end up rebuking in the name of Jesus while you are dying.
For ordinary senses you see a snake enters inside you screaming in the name of Jesus to die without striking him.
You have to apologize while you hit him, the principle of anything that lives for a widow should be born for that life is intelligent.

God will only help you to harm you but to beat him is your responsibility and to know where you missed knowledge because our warfare is in the spirit world.
Even Jesus there were days wanting to stone him but he ran away and hid.
He had the power to do anything but he was making us the principle that even though you are saved and Jesus is in you still have to use the mind and look at the times the Bible says he had run for hours at his beaten hour it was not yet.

So if you do not use your mind properly, it's likely to live a life that you should not live in.

2 CORINTHIANS 4: 4
in whom the god of this world has blinded the minds of the unbelievers, not to shine on the light of the gospel of the glory of Christ, who is God's image.

****************

God has given Satan the name of the god of this world in the way he plays with the minds of men.
Satan does not use force but only plays with your understanding.
He knows exactly when he blinds your mind then the mind will sleep and you will not know God because without sense you will not be able to love God.
Remember God has said to love him with all your mind.

Now he's blinding your thoughts and eyesight in front of you.

So the first characteristic of a person who has not yet been saved and loving God is that he has no sense and his thinking is blinded.

The light of the gospel is not so so even if you preach to him he will not understand because he does not have the mind to meditate on the Word so that the Spirit can heal him.
Even if you want to pray for this person you should pray for his mind.
You'll be talking about Jesus Christ but he does not have the discernment to know how Jesus is found but he is ignorant in it to try to contradict God's mind.

LUKE 24:45
Then He opened their minds to them to understand with Scripture.

**************
Though the mind is not used properly you can not understand the text.
To know the power of the mind as he looks here.

Remember Jesus as he ascended to heaven He said He would send to us the Holy Spirit to teach us and to remind us.
And that Spirit was in him too.
They talk without that Spirit we can not understand or remember.

And here he revealed to them their mind had not yet left, so the Spirit was not in them.
But when they were revealed their minds understood the scriptures.
So he could because the Spirit was in him, but without understanding they did not understand it.

BOOK 13: 30-33
And Caleb stilled the people before Moses, and said, Let us go down quickly, and we will be consumed; for we can overcome it.

But the men that went up with him said, We will not go up against this people; for they are stronger than we.

And they brought the evil tidings of the land unto the children of Israel, saying, The land which we passed through to spy it out, is a land that forsaken the inhabitants thereof; and all the people we saw in it are too long.

Then we saw Nephilim, the sons of Anakim, who came from the Nephilim; and we considered our souls to be as grasshoppers; and so did they see us.

**************

Here were 12 people who went to spy out the country and were all traveling together.
Nobody saw anything different than the other but only two saw the difference although the things they saw were the same.

Caleb says we can win but some say we can not find people there and consider their souls like grasshoppers.

The people who found them did not tell them that they were grasshoppers but they themselves saw the grassland and when they saw the rice they looked really green.

ACTS 23: 7
For what he sees in himself, so is he. He says to you, 'Eat, drink,' but his heart is not with you.

******************
Do you know why these people brought different answers?

The ten who brought the bad news only looked at the mind when they did not see it spiritually.

Both looked spiritually and mentally as well.
They saw them taller mentally but spiritually did not seem to be something.

READING 4: 2
For, indeed, we have been preached the good news, as well as them. But the word that was heard was not good for them, because it was not confused with faith in those who heard it.

***************
They all heard God as He told them that He would conquer them but only those who did not believe in faith were the ten and those who received their information.

There they used intelligence but did not rely on God and relied on Him.

Since the other ten now did not use their minds as well as obey God so they did not inherit the country.
They all died in the wilderness because of not participating in the Spirit and the Spirit.

THAT IS A REQUIREMENT OF THE FUNCTIONS TO FIND EFFECTS.

FROM 18: 19-23
Listen now to my word, and I will give you advice, and God will be with you; Be thou in the presence of the people before God, and bring their words unto God;

and you will teach them the commandments and the law, and you will show them the way it should go, and the work that they should do.

Moreover you will find out of these men a people of valor, godless, true men, haters of dishonest gain; and set them over them, captains of thousands, captains of hundreds, captains of fifties, and captains of tens;

and let them rule over these people at all times; then, every great word shall bring unto you: but every word shall be cut short of them; then you yourself will find more space, and they will take the burden with you.

That you will do this, and when God commands you, then you'll be able to stand up for you, and all these people will go to their place in peace.

***************
This is Jethro his brother Moses was instructing Moses after seeing the Israelites come together to teach them and solve their problems.
For as many as Moses was, he was hated.

Musa is a real man of God but here he is not intelligent to use it because he is given counsel and help him.

It's intelligent used and that's why even today we have only one representative in the parliament we do not go all.

That is why there are representatives of the President who are regional heads and district officials and ministers.
All of them are Functional Offices but intelligence was used so that the country's development could be swift.
Unless you use the mind you will find yourself fit with something you had to complete today when you ended up in the war.

These machines that help us to simplify the work we would not have had without mind and God enabled us.

Now if this Moses did not find this advice he could not completely solve all the problems of the children of Israel because they were too numerous and that they would begin to blame him for his abhorrence in the desert.

PROVERBS 28:16
The head of the poor fails to see a lot of people, but he who wishes to increase his days.

****************

When you become superior and then just lost and the mind is to let the people down.
You may be a Presiding officer or a leader in the office and you really want your citizens the President or your staff to lead a good life but the problem is lacking in mind.

This Moses was eager to quickly solve all the problems of the children of Israel but he did not get the idea of ​​making the people in such a way.

Anarchy solves people's problems all the time in the desert without success.
So even if you see your leader gives you a sense of humor for you to build up his mind.
Even if you are a father in the family, he or she sees the wife and the children you are thinking about.
They do not want to see them unless they have enough mind to satisfy them.
Families need intelligence to lead when a father misses the mind everything is damaged because he is the head.

1 Peter 3: 7
Likewise, ye husbands, abide with your wives in mind; and to give her the honorable wife, as a weaker vessel; and as joint heirs of the grace of life, that your supplication may not be hindered.

*****************

Especially we who are pulling here should really think.
I am a man I should pray for my wife.
Now how will I pray if my mind does not show me to pray for it?
You should pray for him but use the mind to stay with him.
You are not told to stay with a woman only spiritually but also mentally.
You can not only look at the wife's return home and some things that she's going to get out of touch or she is slow to go back and just give her a feeling that she's saved.

You ask God to give you a good wife then you find a woman feeling God has given her a story as a loved one is saved and you stay in the mirror just do not use the mind to explore.

When God wants you to pray for a wife / wife you should use the mind to know what I should apply for her.
That which you will not be aware of in your mind is where God comes with his mind and power to reflect his glory.

What do you want God to tell you when you see a woman wearing pants and clothes that you really do not have a good idea?
DO YOU HAVE A CARE TO FIND YOUR EARLY WORDS?

Use intelligence and meditate on God will help you.
There is a time to please the wife / husband and the time to build up spirituality too.

The issue of pleasing one's marriage and satisfying is not spiritual but the mind should be used.

PSALM 4: 4
Be afraid and do not sin, look at your bed and sit down.

**************

To be afraid and not to sin you must meditate on your mind.

Your mind will tell you to listen to God and God will give your mind the ability to meditate on divine mind and you will find a favorable answer before him.

ACTS 24: 30-34
I went by the lazy field, And the vineyard of the senseless man.

No! Lot also sprouts thorns; his face is covered with worms, and his stone wall is broken.

And when I looked and thought so much; I saw, I got the doctrine.

They're still a little sleep, a little sleep, They're still folding hands to sleep!

Therefore, your poverty comes like a sorcerer, And your need as an armed man.

*****************

Check out this field of the senseless person.
If you do not mind it will grow and you will not reap.

The effect of the senseless person is this.

Poverty comes like a robber.
The robber is the one who is coming to catch you with what you have.
So you will have many needs without help because you do not understand.

An armed man can not prevent him from invading you.
So your important needs will come to you with the power you do not want to do because you do not understand.

This lazy person is said to have no intelligence but is not called God.
Now he may have God but the mind does not.
You can not be greedy of God and then ask God to do the field for yourself.
Your minds will tell you that this is a time to grow and this is a harvest time and this is time to plant or gather the barn.
All these times are available to use them according to their circumstances.
This lazy person will have to die hungry for misuse.

2 Thessalonians 3:10
For even when we were present to you we gave this command, that if anyone does not want to work, then let him not eat food.

******************

Paul then tells them if anyone does not want to work, then let him eat no food.
He did not say if someone does not want to be saved,
He did not say if anyone does not want to fear God.

And that Work you will do with intelligence is not like that lazy one.
Growing time to grow up with the time for prescription and fertilizer to do so.
Using your mind wisely you will win and you will not be poor.
IMPLEMENT OUTSIDE GOD.

ISAIAH 40:28
I am You did not know? Do not hear? The eternal God, the LORD, the Creator of the ends of the earth, is not endless, neither is he consumed; his mind is unsearchable.

*****************
Remember there is a lesson we learned about the title called
MAN'S FOOD (MOST)

We saw how we have become partners of God's divine character.
God says his mind is uncertainty and we are partners of his character and his example.
So when you are with God your mind will not be normal and that's why we have the ability to overcome all the tricks of the Evil One.

2 Corinthians 10: 5
we wipe away the thoughts and everything that rises, the focus on the knowledge of God; and we rob ourselves of every thought to obey Christ;

*****************

Anything that exalts itself than the knowledge of God that he has put in us we have the ability to resist.

What is upbuilding against education is the creation, pretending to be more conscious, ignorant, and miserable.

God has knowledge and also uses intelligence in his performance.

ACT 1: 2
And the land was desolate, and no void, and darkness was upon the face of the waters of the sea; The Spirit of God rested upon the face of the water.

*****************

The Spirit of God rested upon the face of the water and then the word began to work and all that was on the earth and the future came to pass.

But now in the creation of all there are things that were used.

READY 38:33
I am Do you know the commandments commanded to heaven? Can you prove his authority over the earth?

****************

There are orders that are commanded and the heavens become as they are now.
And this is the question God was asking Job on his day of trial.
He asked him to be completely aware of something that Job could not be aware of.
But now look what was used until the sky became as it is.

ACTS 3: 19-20
By wisdom the LORD laid the foundations of the earth: by his understanding he made the firm heaven;

By his knowledge the windows were divided: and the clouds dropped the dew.

*****************

Be careful here,
When the Spirit of God came down upon the depths of the waters he began to pronounce and the word to form.
But the word that Jesus was when he formed was using HAS to establish the foundations of the land,
And by using his solid strings he made the firm heavens.

For her essays the windows were split.
It's as if God used intelligence though he is powerful that you expect to have spiritual strength then do not use intelligence to be done?
There are people in the churches who know the word, they are good applicants, they cast out demons in the name of Jesus but the mind of achieving they do not have.
But that is not God's plan to grow spiritually and to be poor.

3 JOHN 1: 2
Dear friend, I want to be successful in all things and to have your health, just as your soul is doing.

**************

God wants us to be successful in all things.
Spiritually, physically and every kind of success.
In our prosperity we should use the various things God has put in us.

God put the brain in it not a cosmetic but used what he put into it.

Man has been given very great things.
Despite the various objects and globalization you see here on earth, man still has not used even a quarter of the ability of the mind that God has put in it.
No one on earth has spent 50% of the percentage of 100% of the human mind that God has placed in humans.

In order to use your mind you need to ask God to open your consciousness, the memory of the brain let you know and our God is faithful you will be able to use your mind to succeed.

And do not say you're smart, you still do not mind.
When you make a specific prayer, pray for your mind then open and then you will be diagnosed or unwise.
No fool knows that he is stupid.
But those who exceed the mind are the ones who seem to be stupid.
Even the fool and his stupidity are more intelligent and they see him intelligent.

Go before God confessing that you do not understand and ask him to give you knowledge and understanding to teach you for the benefit.

ASAN AS THE HOLY HOLY SPIRITUALLY YOU ARE SPIRITUALLY IF YOU HAVE BENEFICIAL, YOU SHOULD HELP ME TO HELP YOU.

GOD IS EVANGELIZED.
#Powered_By_Holly_Spirit

5 comments: