Wednesday, 16 May 2018

MALANGO/MILANGO

BWANA YESU ASIFIWE

Napenda nikutakie mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako mtu wa Mungu.
Lakini ndani ya wewe kupata mafanikio inabidi uzijue baadhi ya Siri ambazo Roho atazifunua kwetu leo.

Inabidi kwanza ujue kwamba kila mafanikio ambayo yanakuja kwako kuna mlango ambao huwa yanapitia ili kukufikia na ni kusudi la Mungu wewe ufanikiwe.

3YOHANA 1:1-2
Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.
Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.

***************

Hizi ni baraka ambazo Yohana alikuwa akimbariki mzee Gayo ambae inaonekana alikuwa amefanikiwa kwenye mambo ya kiroho lakini kimwili bado.
Hivyo Yohana akawa anamtamkia baraka zidhihirike katika ulimwengu wa mwili.

KWANINI ALIKUWA HAJAFANIKIWA KIMWILI?
Ule mlango ambao baraka na mafanikio yake ilitakiwa yapitie inaonekana adui alikuwa amesimama kuhakikisha anazuia mafanikio yake kimwili kama vile, afya, elimu, maendeleo n.k
Napozungumza kuhusu mafanikio ni zaidi ya pesa, majumba na magari.

Maana unaweza ukaona watu wanamiliki hivyo vyote lakini bado ni mgonjwa wa maradhi yasiyotibika.
Mafanikio anayotakiwa kufanikiwa mtu yaliyo kusudi la Mungu ni kumiliki vyote na kuwa na uzima wa kiroho yaani maelewano mazuri wewe na Mungu.

MALANGO

MALANGO yako yanapomilikiwa na adui huwa anapitisha mambo yake kama magonjwa, umasikini na mengine yote yanayotesa maisha ya binadamu.
Pia yanapofungwa hutaweza kupata chochote maana yatakuwa hayapitishi chochote.
Chochote kile kinachokutokea ukakiona kwa macho yako ni lazima kiwe kimepitia kwenye hayo MALANGO katika ulimwengu wa Roho ndipo yadhihirike katika ulimwengu wa Mwili.

MATHAYO 16:18-19
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lolote utakalolifungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.

********************

Hayo ni maneno Yesu alikua akimwaambia Petro.
Kwamba kanisa atakalosimamisha yeye halitashindwa na MILANGO ya kuzimu.
Kanisa ni mimi na wewe rafiki. Yesu anasema hatutashindwa na vita ya kuzimu maana ametupa sisi funguo za kufungua hiyo MILANGO iwe wazi na baraka zipate kuingia.

MILANGO au MALANGO yako ikishamilikiwa na adui kamwe hutaweza kuona baraka zozote katika maisha yako.

MWANZO 22:17
Katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani, na uzao wako utamiliki MLANGO wa adui zao.

****************

ZABURI 115:10
Enyi mlango wa Haruni, mtumainini BWANA; Yeye ni msaada wao na ngao yao.

********************

ZABURI 24:9
Inueni vichwa vyenu, enyi malango,
Naam, viinueni, enyi malango ya milele,
Mfalme wa utukufu apate kuingia.

***************

Kwa hivyo vifungu hapo juu nadhani utakuwa umeshapata picha juu ya uhusiano wa malango na upitishwaji wa baraka zako.

MALANGO au MILANGO yako inatakiwa iwe wazi na pia anaetakiwa kuwa hapo kama msimamizi ni mfalme wa utukufu ili apitishe mambo mema katika maisha yako.
Tumeona kabisa Mungu alivyomwaambia Ibrahimu kwamba mlango wake utamiliki mlango wa adui.

Pia Haruni anaambiwa mlango wake umtumaini BWANA.

ISAYA 60:11
Malango yako nayo yatakuwa wazi daima;
Hayatafungwa mchana wala usiku;
Ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa,
Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao.

******************

MILANGO yako inatakiwa iwe wazi na imtumainie Mungu.

Na pia tumeona hapa kuwa agano la kumiliki milango Mungu analifanya na Ibrahimu

Kwanini amefanya hilo agano na Ibrahimu?

Mungu amefanya agano na Ibrahimu kwamaana yeye ni mwaanzilishi wa taifa la Israeli.
Kwahiyo rafiki yangu katika maisha yetu sisi ni uzao wa Ibrahimu kiroho.
Tunatakiwa kabisa kuzirithi baraka za Ibrahimu.

Tunaona Ibrahimu anafanikiwa.

Isaka anafanikiwa.

Yakobo anafanikiwa.

Huo ni ukoo wa Ibrahimu ambao mwanzilishi wa huo ukoo ambae ni yeye huyo Ibrahimu MALANGO yake yalimtumaini Mungu.

WEWE MWAANZILISHI WA UKOO WENU ALISIMAMISHA NINI KWENYE MILANGO YENU?
 ALIMTUMAINI NANI?

Haruni aliinua kichwa ili mfalme wa utukufu apate kuingia.
Je, kwenye ukoo wenu mwaanzilishi aliinua vichwa ili nani apite?

ALICHINJA MBUZI?

ALIOMBA MIZIMU?

ALITAMKA MANENO GANI?

Hilo ni swali la kujiuliza.

Omba Roho mtakatifu akufunulie maana yeye huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu.

TUNATOKAJE?
Yesu alishasema hatakubali kanisa lake lishindwe na milango ya kuzimu,
Na kanisa la Kristo ni mimi na wewe tuliyempokea.
Hatutashindwa juu ya hiyo milango ya adui ya huko kuzimu ya kupitisha uharibifu kwa watu wake.
Tuna funguo za kufunga na kufungua ambazo ni yeye mwenyewe.

YESU NDIYE FUNGUO.
Kama umempokea na yeye akakaa ndani yako atafunga na kufungua na atafungua milango yako na kufunga ile ya kuzimu.

Haya yote ni mambo ya rohoni na hayaonekani kwa macho ya nyama.
Kuzimu ni ufalme ambao anaishi shetani na milango ya shetani ipo na inapitisha laana na uharibifu wake wote.
Lakini pia upo ufalme wa Mbinguni ambao ni wa Yesu Kristo na mlango wa huko mbinguni ni Yesu Kristo pekee.

Hivyo hizo falme mbili huwa zinafanya kazi kwetu sisi.
Ufalme wa mbinguni ukitubariki na kuzimu ukitulaani.

Tunamshukuru Mungu baba kwa jina la Yesu Kristo kwani ametupa mamlaka ya kuharibu na kuvunja ngome zote huko kuzimu.

WAEFESO  6:11-17
Vaeni silaha zote za Mungu, Mpate kuweza kuzipinga hila za shetani.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; Bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu.

*******************

WOKOVU TUNAO, SILAHA TUNAZO, FUNGUO TUNAZO NA MAMLAKA PIA TUNAYO

Tunasubiri tena nini watu wa Mungu?

NAWATAMKIA BARAKA ZOTE KWA JINA LA YESU KRISTO.

AMEN.

POWERED BY HOLLY SPIRIT

2 comments:

  1. Ubarikiwe mtumishi wa Mungu, somo nimelielewa.

    ReplyDelete
  2. Amina sana Mtumishi Hilo NI kweli na hakika Sana!

    ReplyDelete