Saturday 12 May 2018

OMBA HALAFU CHUKUA HATUA USISUBIRI MUUJIZA.

BWANA YESU ASIFIWE SANA

ASANTE SANA ROHO MTAKATIFU KWA KUNIFUNULIA MIMI MTOTO MCHANGA NA KUWAFICHA WENYE HEKIMA NA AKILI ZAO.

1WAKORINTHO 1:18-19
Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.

 Kwa kuwa imeandikwa,Nitaiharibu hekima yao wenye hekima,Na akili zao wenye akili nitazikataa.
"
"
"
LEO ROHO MTAKATIFU ANATUFUNDISHA NENO LENYE KICHWA KINACHOSEMA.

OMBA HALAFU CHUKUA HATUA USISUBIRI MUUJIZA.

Hili nambo la kuchukua hatua limekuwa ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaomwamini Mungu.

Uwezo wa kufanya chochote tena katika mazingira yoyote upo kwa Mungu wetu wa mbinguni lakini Mungu anapenda sana uchukue hatua.

Ndiyo maana hata yeye katika kutuletea WOKOVU anasema

YOHANA 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu alivyoupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, Bali awe na uzima wa milele.
"
"
"
Mungu angeweza kusema tu kwa maneno kwamba

 "NIMESHAWAPA WOKOVU"

Lakini alichukua hatua na ikaonekano mbele za macho ya watu.

TWENDE KWENYE MSINGI WA MAFUNDISHO YETU YA LEO.

YAKOBO 2:17
Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
"
"
"
Usikae tu ukimuomba Mungu kwa imani bila kuchukua hatua ya kuufuata muujiza unaoutafuta.
Wana wa Israel wasingeweza kusimama pale Misri kwa imani halafu wakajikuta wapo nchi ambayo Mungu aliwaapia baba zao kwamba itakuwa yao.

Usije ukakaa ukimuomba Mungu akupe kazi ya kulipwa mshahara mkubwa na wakati huna hata juhudi za kuitafuta yenye mshahara mdogo.

Usije ukamuomba Mungu kwa imani yako akupe Mume/Mke mwema na wakati wewe ni waruwaru.
Yani unataka mtu mkarimu na mstaarabu na wakati wewe ni mchoyo na hujatulia.
Kumbuka Mungu alisema atakupa wa kufanana na wewe.

CHUKUA HATUA
Wana wa Israeli bila kuchukua hatua wasingeirithi ile nchi.
Wana wa Israeli mpaka kuifikia ile nchi ya ahadi walikutana na vikwazo vingi sana njiani.
Mungu alikuwa anaviona lakini aliviacha ili watakapochukua hatua ya kupambana navyo nae aingilie kati kuwasaidia.

YOSHUA 24:7-8
Nao walipomlilia BWANA, akaweka giza kati ya ninyi na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi.

 Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori waliokaa ng’ambo ya pili ya Yordani; nao wakapigana nanyi; nikawatia mikononi mwenu, mkaimiliki nchi yao; nami nikawaangamiza mbele yenu.
"
"
"
Jambo lolote unalotaka Mungu akutendee pamoja na kuomba inatakiwa uchukue hatua.
Sasa wewe kaa nyumbani halafu umuombe Mungu kwamba unatafuta kazi utaona matokeo yake.

Wewe kijana endelea kupanga wanawake foleni ukifikiri ni sifa au kuna tunzo utapata halafu umuombe Mungu akupe mke mwaminifu ukifikiri kuna muujiza utatokea.

Na wewe msichana endelea kuvaa nguo zisizo na maadili kabisa na kubadilisha wanaume kila siku huku ukimuomba Mungu mwanaume mwenye akili zake timamu ufikiri kuna muujiza utatokea.
Ukikaa mahali popote unaongelea ngono tu na maneno machafu yanatoka kwenye kinywa hichohicho unachokitumia kumuitia Mungu kwenye matatizo yako.
"UTAMPATA WA KUFANANA NA WEWE"

Kila jambo unaloliombea lazima uchukue hatua ndipo Mungu nae ataingilia kati.

KUTOKA 14:13-14
Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.

 BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
"
"
"
Tazama hapo Musa amewajengea imani ambayo Mungu hakukubaliana nayo.
Alivyowaambia "simameni tu"
Kumbe japo Musa alikuwa na imani sana na Mungu kwamba lazima atawaokoa lakini hakupaswa kuwaambia wasimame.
Angalia Mungu alichomwambia Musa baada ya kuwaambia wana wa Israeli "simameni tu"

KUTOKA 14:15-17
BWANA akamwambia Musa, Mbona unanililia mimi? Waambie wana wa Israeli waendelee mbele.

 Nawe inua fimbo yako, ukanyoshe mkono wako juu ya bahari, na kuigawanya; nao wana wa Israeli watapita kati ya bahari katika nchi kavu.

 Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake.
"
"
"
Kwa imani Musa aliwaambia "simameni tu"
Lakini Mungu akamwambia Musa "mbona unanililia mimi? "Akiwa na maana kwamba hakutakiwa asimamishe wale watu.
"Waambie wana wa Israeli waendelee mbele"
Mungu hataki mtu asimame, aache kuchukua hatua kwenye jambo lolote awe anamlilia yeye.
Mungu anasema kabisa atajipatia utukufu kwa farao pindi wana wa Israeli watakapopita kwenye njia kati ya bahari.
Ataifanya mioyo ya wamisri kuwa migumu.
Na hapo walipowafuata ndiko kulikokuwa kuangamia kwao na kweli Mungu akajipatia utukufu.

Hata wewe unapomuomba Mungu jambo lolote kwa imani ni lazima uchukue hatua mtu wa Mungu.

CHUKUA HATUA UTAONA MUNGU ANAVYOFANYA KAZI KUBWA SANA KATIKA MAISHA YAKO.

Kuna mambo ambayo huwa unamwomba Mungu wewe unafikiri bado hajakujibu ila ni kwa vile hujafuatilia ndipo akuonekanie katika jitihada zako.

HESABU 13:32-33
Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nchi waliyoipeleleza, wakasema, Ile nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nchi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno.

 Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi.
"
"
"
Wale walioenda kuipeleleza ile nchi waliwaletea habari mbaya ambazo ni za kishetani ili wasiende.

Kuna namna unataka kujaribu lakini unajiona wewe si chochote katika hilo jambo unalotaka kulifanya.
Unaanza kujiona dhaifu unaogopa.

Waliwaletea habari za ile nchi kwamba walipowaona hao Wanefili wana wa Anaki waliotoka kwa hao wanefili walianza kujiona nafsi zao kama mapanzi nao wakawaona hivyo hivyo.

METHALI 23:7
Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.Akuambia, Haya, kula, kunywa;Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
"
"
"
METHALI 18:21
Mauti na uzima huwa katika uweza wa ulimi, na wao waupendao watakula matunda yake.
"
"
"
Jinsi unavyojishusha na kuogopa kuchukua hatua ya kufuatilia kile unachomuomba Mungu ujue ndivyo unavyoshushwa pia.

HESABU 14:9
Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; uvuli uliokuwa juu yao umeondolewa, naye BWANA yu pamoja nasi; msiwaogope.
"
"
"
Ona sasa kumbe kile wanachokiogopa wao ni chakula chao.
Usitishike na majira na nyakati ngumu katika maisha yako.
Usiangalie watu wanasema nini ili kukuvunja moyo katika jitihada zako.
Haya mambo yalikuwepo tangu zamani.
Yupo Mungu mbinguni anayetutia nguvu wewe chukua hatua, amka uifuate ndoto uliyoiota.

KUTOKA 23:27
Nitatuma utisho wangu utangulie mbele yako, nami nitawafadhaisha watu wote utakaowafikilia, nami nitawafanya hao adui zako wote wakuonyeshe maungo yao.
"
"
"
Kwanza unapomwendea Mungu usiangalie ukubwa wa tatizo ulilonalo,
Bali angalia na kutafakari ukubwa wa Mungu unaemwamini katika hiyo changamoto yako.
Muombe Mungu kwa imani kwamba unataka akupe kazi kwenye ofisi fulani halafu chukua hatua nenda pale kaombe kazi.
Usiwaogope hao Wanefili wana wa Anaki waliotoka kwa hao Wanefili.
Utawakuta hapo lakini ujue hao ni chakula kwako.
Usijione kama panzi mbele yao maana nao watakuona hivyo hivyo.

Mungu ameshawafadhaisha na kuvifadhaisha vyote katika kumuomba kwako lakini tatizo lipo kwako hujachukua hatua ukawafikia na utisho tayari upo mbele yao.
Chukua kibali chako nenda kwa kujiamini ukiwa na matumaini na Mungu wako halafu utauona wokovu wake BWANA wa Majeshi akijipatia utukufu wake.

Usiogope ukubwa wa ofisi

Usiogope ukubwa wa meneja mwajiri

Usiogope suti zao

YAMKINI CHANGAMOTO YAKO NI UGONJWA

Usiogope ukubwa wa ugonjwa

Usiogope majibu ya daktari maana hayazidi majibu yatokayo kwenye kiti cha enzi kwa Mungu wetu.

Jina la Yesu linazidi jina la ukimwi

Jina la Yesu linazidi jina la kansa

WAFILIPI 2:9
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;
"
"
"
Kwa jina la Yesu hakuna jina liwalo lote linaloweza kusimama na kushindana nalo.
Jina la Yesu linazidi majina yote.

Ni shetani anakupa utisho tu na kukuambia hii ofisi kubwa hivi usiingie wala hutapata msaada.

Huu ugonjwa mkubwa hivi wala usihangaike kutafuta uponyaji maana hutapona

Au vitu kama hivi siyo saizi yako waachie watu fulani maana utavihangaikia bure wala hutafanikiwa unapoteza muda wako.

METHALI 3:4-5
Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,
Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe.
"
"
"
Unatakiwa umtumaini BWANA kwa moyo wako wote na uwe na imani kwamba anaweza Jambo lolote.
Pia utumie akili maana yeye anasema

ISAYA 48:17
Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.
"
"
"
Kwanini Mungu anasema anakufundisha ili upate faida?  Inamaana utazitumia hizo akili na maarifa anayokupa.
Akili nzuri anayokupa Mungu inabidi uitumie.
Mbele zake na mbele ya mwanadamu ili ufaidike.

Unapaswa kutumia sana akili zako pamoja na kumtumaini Mungu.
Lakini hupaswi kuzitegemea kabisa hizo akili maana anasema pia amezikataa akili zao wenye akili na hekima yao wenye hekima ameiharibu.

"TUMIA AKILI NA MAARIFA YAKO YOTE LAKINI USITEGEMEE VITU HIVYO MTEGEMEE MUNGU."

Kila mtu aliyemtumaini Mungu alishinda baada ya kuchukua hatua.

ESTA 4:15-17
Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,

 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.

 Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote kama vile Esta alivyomwagiza.
"
"
"
Esta anawaambia watu wafunge na kuomba ili Mungu awaokoe wayahudi na hukumu iliyokuwa mbele yao.
Lakini pia Esta anasema atachukua hatua ataingia kwa mfalme kinyume cha sheria.
Siyo kwamba aliomba tu kwa imani na kusubiri ule waraka wa Hamani ubatilishwe kimuujiza.
Namna ambayo Esta alitaka kuingia kwa mfalme siyo rahisi kama unavyofikiria ndiyo maana Esta anasema kinyume cha sheria na akiangamia na aangamie.
Lakini ilibidi achukue hatua ili BWANA ampiganie.

ESTA 5:2-3
Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.

 Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme.
"
"
"
Tazama baada ya Esta kuingia uani kwa mfalme ndipo mfalme alimwona akapata kibali machoni pake.
Kitendo cha kumwona tu Esta akapata kibali machoni pake.
Je, asingemwona angepata kibali?

ESTA 7:1-10
Basi mfalme na Hamani walikuja kula karamu pamoja na malkia Esta.

 Mfalme akamwambia Esta tena siku ya pili pale pale penye karamu ya divai, Malkia Esta, dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa.

 Ndipo malkia Esta alipojibu, akasema, Mfalme, ikiwa nimepata kibali machoni pako, na mfalme akiona vema, nipewe maisha yangu kuwa dua yangu, na watu wangu kuwa haja yangu.

Maana tumeuzwa, mimi na watu wangu, ili tuharibiwe, na kuuawa, na kuangamia. Kama tungaliuzwa kuwa watumwa na wajakazi, ningalinyamaza; ila hata hivyo msiba wetu haulinganishwi na hasara ya mfalme.

 Ndipo mfalme Ahasuero aliponena, akamwambia malkia Esta, Ni nani huyu, tena yuko wapi, ambaye moyoni mwake alithubutu kufanya hivi?

 Esta akasema, Ni mtesi, tena ni adui, ndiye huyu Hamani, mtu mbaya kabisa. Mara Hamani akaingiwa na hofu mbele ya mfalme na malkia.

Mfalme akaondoka katika ghadhabu yake kutoka kwenye karamu ya divai, akaingia bustani ya ngome. Hamani naye akasimama ili ajitakie maisha yake kwa malkia Esta; kwa kuwa aliona ya kwamba amekusudiwa madhara na mfalme.

 Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hata mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema, Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani.

Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake.

 Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.
"
"
"Maombi ya Esta na wayahudi Mungu aliyasikia sana.
Hatua za Esta zilimbadilishia kifo cha Mordekai.
Hamani akaangamia kwenye mti aliomwandalia Mordekai kutundikiwa.

Ukikaa vizuri na Mungu na ukilijua neno lake linasema nini huwezi kuangamia kwa jina la Yesu.
Wewe unaamua mwenyewe je,
Hao wachawi unataka uangamize uchawi wao?  Au unataka walichotuma kwako uwarudishie waangamie wenyewe?
Au unataka uzuie kabisa na kupiga marufuku nguvu zozote za kichawi kukufuatilia?

Kila unachotaka kukifanya hapa duniani majibu yapo kwenye BIBLIA yako.

NAKUTAKIA MWANZO MPYA NA USHINDI WA KISHINDO KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
USIANGAMIE KATIKA MITEGO YAO.
MASHIMO WALIYOKUCHIMBIA WAKADUMBUKIE WAO WENYEWE.
ANZA SASA KUCHUKUA HATUA HUKU UKIMTUMAINI YEYE NA HAUTA AIBIKA MILELE.
NIMEOMBA NIKIAMINI NA KUSHUKURU KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
AMINA.

#Powered_by_Holly_Spirit

2 comments:

  1. Amina sana mtumishi, nimebarikiwa sana

    ReplyDelete
  2. Amen mtumishi wa Mungu hakika somo hili limenifungua kwa kiasi Cha juu mno

    ReplyDelete