Sunday 9 September 2018

AINA YA IMANI INAYOWEZA KUKUSAIDIA

NAKUSALIMU KWA JINA LA YESU KRISTO

Sifa na utukufu ni kwake YESU KRISTO aliyeachilia kibali na kuufanya huu uwe wakati mzuri kabisa uliokubaliwa kwaajili ya kujifunza tena NENO lake.
Tunasimama kinyume na kila mpango wa adui wa kupofusha fikra za watu kulielewa hili somo na kutiisha kila fikra ipate kumtii KRISTO kuanzia sasa.
IN THE NAME OF JESUS CHRIST
AMEN

Leo tunajifunza somo lenye kichwa kinachosema,

AINA YA IMANI INAYOWEZA KUKUSAIDIA

Lengo la Roho Mtakatifu kutufundisha somo hili ni kusaidia kujuwa kwamba hata kama una imani kubwa kiasi gani ni kwa jinsi gani inaweza kuwa msaada kwako, maana unaweza ukawa na imani kubwa sana lakini usipofahamu ni kwa namna gani hiyo imani yako imejengeka au ulivyoijenga bado haitakuwa msaada kabisa kwako.
BWANA YESU ASIFIWE SANA.

WAEBRANIA 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

**************
Hii haijalishi kwamba wewe uko katika dini gani, au hauna dini kabisa au haijalishi unamwabudu nani lakini tafsiri ya imani ndiyo hii.

Kuwa na imani ya namna hii iliyojengeka katika misingi ya matendo fulani itakupa uwezekano wa hilo jambo unaloamini kutokea kwakuwa unavyo vigezo.

Lakini hapa leo nazungumzia imani ya kumwamini Mungu kupitia neno lake.
Ni kwa namna gani tunaweza kujihakikishia kwamba tuna imani inayoweza kutusaidia kwa kusikia neno?

YAKOBO 2:19
Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

****************
Ukweli ni kwamba kila kiumbe hai chenye akili timamu huwa kinaamini kabisa kwamba Mungu ni mmoja na hashirikishwi na chochote tena hashindwi kufanya lolote kwa wakati wowote.
Sasa kuna watu wanasema kwamba wao hawana haja ya kujuwa mambo mengine zaidi kuhusu imani yao bali wanachokiamini tu wao ni kwamba Mungu yupo.

Lakini wanachokiamini wao na mashetani wanachokiamini ni kitu kimoja kwa mujibu wa maandiko au neno la Mungu.
Unamwamini Mungu kwamba ni mmoja; unatenda vyema sana, ila ujue hiyo imani yako ni sawa na ya shetani tena huyo shetani anakuzidi kwa imani maana yeye anamwamini mpaka anatetemeka.

Shetani anamwamini Mungu kwamba ana nguvu na wala hawezi kujaribu hata kushindana naye na ndiyo maana anaelekeza hasira zake kwetu ambao ni watoto wa huyo Mungu.
Naye Mungu akatupa sisi silaha ya kumpinga ambayo ni jina la Yesu kupitia kuokoka.
Na hilo jina tukilitumia vizuri ni lazima tumshinde, lakini sasa shetani anakupofusha fikra wewe usiokoke maana anajuwa utakapo okoka tu utakuwa na haki ya kumtiisha ya kutumia hilo jina itokayo katika Yesu Kristo ambayo huja kwa neema.
Hakubali kuachia ufahamu wako uamini kuokoka maana atashindwa na itakuwa shida sana kwake.

Sasa wewe unabaki ukikataa wokovu huku ukilitumia jina la Yesu ukiwa ndani ya dini yako ambayo haiwezi kukupa mamlaka ya kulitumia hilo jina.
Unabaki ukisema eti imani yako itakuponya.
Imani inayokusaidia ni ile yenye misingi ya neno la Mungu.

AINA MBILI ZA IMANI

IMANI YA KWANZA

LUKA 8:43-48
Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,

alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.

Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.

Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.

Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.

Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.

**************

Huyu mwanamke alikuwa na imani iliyomuelekeza kwa Yesu Kristo baada ya kumsikia na akamfuata akaugusa upindo wa vazi lake.

Aliamini kwamba Yesu anaponya lakini siyo kuamini tu bali kuna matendo aliyoyafanya mpaka akapokea uponyaji ambayo ni kumfuata na kugusa upindo wa vazi lake.

IMANI YA PILI

MATHAYO 8:5-10
Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,

akamsihi, akisema, Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.

Yesu akamwambia, Nitakuja, nimponye.

Yule akida akamjibu, akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema neno tu, na mtumishi wangu atapona.

Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.

Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.

**************

Huyu akida alimwamini Yesu akamfuata ili amponye mtumishi wake na hapo Yesu akataka kufanya tendo la kumfuata lakini tunaona hapo akida akiwa na imani nyingine tofauti kabisa ambayo ilimshangaza hata Yesu.
Anamwambia asimfuate bali aseme neno tu na mtumishi wake atapona.

Hawa watu wawili wote walikuwa na imani na Yesu,
Lakini imani zao hazikuwa bila matendo na hata matendo yao hayakufanana.
Mmoja aliamini Yesu anaponya lakini kwa kugusa upindo wa vazi lake.
Huyu mwanamke angekuwa na imani kama ya yule akida wala asingegusa upindo wa vazi bali angesikiliza tu neno na angepona,
Maana tunaona akida aliamini pia Yesu anaponya lakini hata kwa neno lake.

LUKA 5:17
Ikawa siku zile mojawapo alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waalimu wa torati walikuwa wameketi hapo, waliotoka katika kila kijiji cha Galilaya, na Uyahudi, na Yerusalemu; na uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya.

*****************

Hata katika mafundisho tu uweza wa Mungu unakuwepo kwa imani ili uponye.
Sasa wewe unayesema kwamba imani yako inakuponya kirahisi tu pasipo maarifa yoyote je, imani yako ipo katika msingi upi?
Wewe ambaye hutaki kuokoka na unajiona unamwamini Mungu huwa unamwamini kwa njia ipi kama hutaki kutii neno lake ukaokoka?
Au imani yako ni kama ya shetani tu kwamba unaamini Mungu ni mmoja huku hutii neno lake?
Wewe una tofauti gani na shetani?
Shetani anaamini Mungu ni mmoja na halitii neno lake.
Wewe nawe unaamini Mungu ni mmoja na hutii neno lake na ndiyo maana hutaki kuokoka.
Wewe una tofauti na shetani? JITATHIMINI.

WARUMI 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

*************

Ili uanze kuwa na imani unatakiwa ulisikie neno la Kristo na kulitii.
Lakini wewe unadai unalisikia neno na wakati hutimizi kile neno linachokuelekeza.

IMANI NI LAZIMA ITOKANE NA NENO LA MUNGU, HALAFU NENO LINGINE LITAKUPA MAELEKEZO YA KUFANYA JAMBO FULANI ILI IMANI ULIYOIPATA KWA KULISIKIA LILE NENO LA KWANZA IKUSAIDIE.

Huwezi kusema tu kwamba imani yako ndiyo itakayokuponya, imani inayoweza kukusaidia ni ile inayokuja kwa kulisikia neno la Kristo.
Imani ziko nyingi ila inayosaidia ni ile imani inayotokana na neno la Kristo.
Na neno la Kristo ni lazima likupe mwongozo wa kufanya jambo fulani ili imani hiyo ithibitike au hilo neno lithihirike kwako.
Kuna jambo la kufanya zaidi ya kumwamini Mungu tu ili imani yetu iwe na matokeo zaidi ya ile ya shetani ambaye naye humwamini Mungu tena na kutetemeka.

YAKOBO 2:17
Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.

******************
Unapoamini kwamba Mungu anabariki ni lazima ufanye matendo fulani kwa mujibu wa biblia ambayo mtu anayetaka kufanikiwa ni lazima ayafanye huku akimwamini Mungu, na matendo hayo unaelekezwa na neno pia.
Unaamini Mungu anabariki na kukufanikisha lakini hata kama hiyo imani yako ni kubwa kiasi gani ni lazima ufanye kazi.

KUMB 28:8
Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.

******************
Ukishamwamini Mungu ni lazima ufanye kazi za mikono yako ili baraka zipitie hapo.
Amesema atakubariki na umwamini lakini siyo kwamba utaokota au utaamka usingizini bali ni lazima ufanye kazi na hiyo mikono yako.
Ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala yako, je kama huna hiyo ghala hiyo baraka itapitia wapi?

Na pia zaidi ya hayo hakuna kazi yoyote ya mikono inayopata baraka za Mungu kama hutoi zaka na sadaka maana kile unachopanda ndicho utakachovuna.

HAGAI 1:9
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.

**************
Wewe ukiambiwa utoe mchango wa ujenzi wa kanisa unahisi unamfaidisha mchungaji.
Hayo ndiyo matokeo yake.
Umeshamwamini Mungu na wewe ni mwombaji, umeshafanya Kazi sawa kama neno linavyokuelekeza na unasubiri baraka lakini Mungu anasema ulitarajia kubarikiwa lakini hubarikiwa maana hujaijenga nyumba yake.
Sasa wewe endelea kusema imani yako inakuponya au itakusaidia nakuambia utaendelea kupasha kiti moto.

HAGAI 1:6
Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka.

*****************
Unashangaa hata ukilipwa mshahara mkubwa kiasi gani lakini kwako madeni hayaishi.
Unakula vizuri lakini huna amani na chakula chako.
Huelewi elewi namna fedha zako zinavyoelekea bali unajikuta tu zimeisha.
Unaanza kukemea chuma ulete na wakati chuma ulete ni wewe mwenyewe.
Imani isiyokuelekeza cha kufanya ni imani hewa hiyo wala haikusaidii.
Hiyo imani yako ya kujiona unajuwa sana ya kusema unamwamini Mungu na hutaki kuokoka ni upepo.

Mungu ameshaweka misingi ya kumwamini kwamba ni lazima upitie kwa njia ya Yesu Kristo.
Vinginevyo ni kujilisha upepo.

YOHANA 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

*****************
kama unatarajia uzima misingi yake ndiyo hiyo.
Kumjuwa au kumwamini tu Mungu haikutoshi bila kumjuwa Yesu Kristo aliyemtuma.
Na Yesu anasema ili uje kwake ni lazima uokoke.

Imani nyingine zinaweza kuwa kubwa sana lakini pasipo matendo ni bure.

NAMNA YA KUAMINI KWAMBA UNAMPENDA MUNGU

1-KUJITENGA NA DUNIA
Hakuna mtu hapa duniani ambaye hasemi kwamba anampenda Mungu.
Tena anaamini kabisa moyoni mwake kwamba Mungu ndiye mweza wa yote.
Anajihisi kabisa kumpenda lakini hiyo imani yake mtu huyo ni hewa wala hampendi Mungu.
Kuna vitu tukiviangalia kwako halafu tukisoma biblia tunakuona humpendi Mungu hata kidogo.

YAKOBO 4:4
Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

*****************
Kama wewe ni mzinzi huwezi kuniambia kwamba unampenda Mungu.
Imani yako ni hewa japo unaamini kwamba unampenda Mungu.
Unaipenda dunia na mambo yake ya ubatili huwezi kuwa rafiki wa Mungu.

WARUMI 12:1-2
Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

*****************
Kuna mtu unamwona kabisa anavaa mavazi ya ajabu yuko uchi ananadi makalio barabarani na kwenye mitandao lakini anakuambia eti nimeokoka nampenda Yesu.
Ukimwuliza juu ya uvaaji wake anakuambia Mungu haangalii mwili.

Ndugu yangu Mungu anaangalia mambo yote hata njia zako.
Unavaa nguo kiasi ambacho ukisimama na mtu ambaye hajaokoka huonyeshe tofauti yoyote halafu unasema umeokoka.
Nakuambia wewe ndiye unaye amini kwamba umeokoka lakini kwako hakuna wokovu.
Mungu angekuwa haangalii mwili asingesema tuitoe miili yetu kama dhabihu iliyo hai tena takatifu na ya kumpendeza.

Unapovaa suruali wewe mwanamke ni kutokujiamini na kuamua kuonyesha kwamba jamani enyi wanaume wa mataifa nioneni maana na mimi nina makalio.
Unasema unampenda Mungu lakini unapingana na maandiko yake?

YOHANA 14:15
Mkinipenda, mtazishika amri zangu.

**************
Huwezi kumpenda Mungu halafu ukatafuta uhalali wa kupinga andiko hata moja kutoka kwenye biblia.

Umeambiwa usiifuatishe namna ya dunia maana unapokuwa umempenda Mungu unakuwa haupo tena ndani ya dunia hii.
Ni lazima uwe tofauti na wale walioko ulimwenguni.

Nasema walioko ulimwenguni maana kama kweli unampenda Mungu huwa unakuwa mbali na ulimwengu na mambo yake.

YOHANA 17:14
Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.

***************
Mimi nakuambia kabisa ukimpenda Mungu huwezi kuunadi mwili wako tena utakuwa na aibu kuvaa nguo ili tu uonyeshe makalio.

Tena inashangaza ukimwambia mwanamke juu ya suruali anapambana kabisa yani analipinga neno lake waziwazi.

DANIELI 3:20-21
Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

Basi watu hao wakafungwa, hali wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na joho zao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya ile tanuru iliyokuwa ikiwaka moto.

***************
Nyie mnaosema kwamba  biblia haijasema kwamba suruali ni vazi la mwanaume je, hawa waliokuwa wamevaa hili vazi ni jinsia gani?
Unafikiria nini juu ya huu mstari?
Tena Mungu mwenyewe ndiye aliyeamua na kulibuni vazi hili na kusema wavalishwe wanaume sasa wewe ni nani hata upinge?

KUTOKA 28:42-43
Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani;

na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.

*************
Kama Mungu amesema haya yawe mavazi ya Mwanamume wewe mwanamke unaanzaje kuvaa?
Huko ndiko kuwa na imani kwamba unampenda Mungu bila kuzishika amri zake.
Ukiamua kuokoka okoka na kama huwezi bado unatamani ya dunia wewe endelea nayo.

WAEFESO 2:1-3
Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;

ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;

ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.

***************
Kama ulikuwa mwovu kwaajili ya hayo hayo ambayo mataifa wanahangaikia inakuwaje unasema umeokoka na bado mwenendo na matendo yako ni kama yale yale?

Wana wa kuasi ni wale walio okoka halafu bado wanaishi maisha yale yale.
Unakuwa tayari uitwe mwana wa kuasi ilimradi tu unyoe kiduku kama hao?

2-UPENDO NA KUJITOA

Ili ujijue kwamba unampenda Mungu au kujithibitishia kwamba unampenda Mungu siyo kuamini tu moyoni mwako hata kama unajihisi una imani kubwa kiasi gani katika hilo.

1 YOHANA 4:8-9
Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.

Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.

****************
Kama huna upendo basi ujijue kwamba huna Mungu wala huyo Mungu humpendi bali ni kutokuwa na ufahamu tu na kushindwa kujitathimini kwamba unampenda nani.

1 YOHANE 4:20
Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.

*****************
Njia pekee tu ya kujijuwa kama unampenda Mungu au humpendi ni kushika amri zake zote ikiwa ni pamoja na hii kwamba uwapende watu wote.

Kama kuna mtu yeyote unayemchukia hapa duniani basi ni tafsiri ya kwamba humpendi Mungu.

IMANI YAKO ULIYONAYO YA KWAMBA UNAMPENDA MUNGU NI LAZIMA IAMBATANE NA MATENDO YA KUWAPENDA WATU KWANZA.

Asiwepo mtu yeyote uliye na chuki naye moyoni mwako, au kisasi, hasira, na mambo mengine yanayofanana na hayo halafu ukajiaminisha kwamba unampenda Mungu.

Pia ili uamini kwamba unampenda Mungu ni lazima ujitolee.

YOHANA 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

***************
Dalili ya kujijuwa kwamba unapenda ni kujitoa,
Kujitoa kwa ajili ya kazi ya Bwana, kujitoa kwa ajili ya wale wenye uhitaji wa mambo mbalimbali.

Ukimpenda Mungu utawapenda na watu unaowaona na kwakuwa unawapenda ni lazima ujitoe kuhubiri injili kwao ili wakutane na Yesu awaokoe.

Ndiyo maana hata Yesu alisema hivi,

MATHAYO 25:34-40
Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;

kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;

nalikuwa uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijia.

Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?

Tena ni lini tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?

Ni lini tena tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?

Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.

*****************
Kama una fedha lakini ni zako mwenyewe wala huna msaada wowote kwa wahitaji kumpenda kwako Mungu kuko wapi?
Una utajiri mpaka wa ziada lakini hujui jambo lolote juu ya jirani au ndugu yako anayehitaji msaada halafu unasemaje unampenda Mungu?
Unajiaminisha tu kwa kujifariji kwamba unampenda Mungu lakini bila upendo kwa wengine unaowaona kwa macho hakuna upendo hapo kwa Mungu usiyemwona.

Unapojiaminisha kwamba unampenda Mungu ni lazima uambatanishe na hayo matendo ili uwe na uhakika na imani yako.

MATHAYO 5:44-48
lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?

Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo?

Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

*****************

Utofauti wako na watu wa mataifa ndiyo utakaofanya hata watu wakikuona wakuogope na kutetemeka na wenyewe wakiri na vinywa vyao ya kwamba kweli wewe ni mtoto wa Mungu au kweli wewe unampenda Mungu.

Ni jambo gumu sana kwa  mtu wa mataifa kumpenda adui yake na kumwombea rehema,
Ikiwa imani yako inakuambia unampenda Mungu basi ni lazima huyo Mungu awe ndani yako na Roho yake itampenda aliyekukosea hata akawa adui kama yeye alivyoanza kutupenda sisi tukiwa bado ni waovu tuliomkosea hata akamtuma mwanaye wa pekee kutupatanisha kwa kuiondoa ile hati ya mashtaka kwaajili yake mwenyewe ili tu tuweze kumkaribia.

Mtu asiye mpenda Mungu humchukia adui yake lakini wewe unayejiamini kwamba unampenda Mungu ni lazima uonyeshe kwa matendo kuwa tofauti naye kwakuwa Mungu aliyeko ndani yako hana ubaguzi.
Ukiona umeshindwa hilo basi ujijue kabisa ni ishara ya kuwa humpendi Mungu na wala hayuko ndani yako.
Ili upate kuwa mwana wa Mungu ni lazima uwapende watu wote kama Mungu mwenyewe kwakuwa yeye amekuwa ndani yako kwa kuwa mwana wake.
Vinginevyo utakuwa unajipa imani ya bure kwamba unampenda Mungu.
Ishara ya kumpenda Mungu ni wewe kuwa mkamilifu na kuwa na viwango vyote alivyo navyo Mungu kwakuwa utakuwa naye mahali pamoja.

Imani yako iambatane na matendo ili kuhakikisha kwamba unachokiamini ndicho au sicho.

MFANO

1 PETRO 3:7-9
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

Neno la mwisho ni hili; mwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;

watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka.

****************

Unaweza ukawa na imani kubwa sana isiyo na mashaka kwamba utabarikiwa wewe na familia yako, yani wewe na mke wako au wewe na watoto na Mume wako.
Lakini ili mrithi hizo baraka kuna vitu mnapaswa kuvifanya kwa vitendo kabisa ambavyo ni hivyo vilivyotajwa hapo.
Kama unaamini kubarikiwa halafu humpi mke wako heshima ujue hiyo imani yako ni bure maana kuomba kwenu kutazuiliwa.

Mnatakiwa kuwa na nia moja, wenye kuhurumiana na kupendana pamoja na unyenyekevu, msiolipizana baya kwa baya na kulaumiana bali mwe wenye kubariki kila mabaya na siyo kuyalaumu na hapo ndio utakapokuwa na imani thabiti kwamba mtarithi baraka.
Na hizo baraka pia ili mzirithi bado mtakuwa na cha kufanya kama kufanya kazi, kutoa zaka na sadaka kwani apandacho mtu ndicho atakachovuna, kuijenga nyumba ya Bwana kama tulivyoona hapo juu pamoja na kujitoa pia kwaajili ya Mungu.
Ukishafanya hayo yote ndipo utakuwa na imani kwamba utabarikiwa, ila vinginevyo imani yako haina matendo hivyo imekufa.

Mfano mwingine ni kwamba mtu mwenye imani ya kuwa atapata mwenzi mwema katika maisha ni yule aliyeanza yeye kuwa mwema kwanza ili ampate wa kufanana naye maama biblia inasema Mungu anakupa wa kufanana na wewe.
Sasa wewe endelea kujiaminisha kwamba utapata mtu mwenye akili kama wewe ni sifuri.

WAKOLOSAI 3:16
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

***************

Neno la Kristo likikaa kwa wingi ndani yako utajuwa kwamba kila imani unayoiamini inakutaka ufanye matendo gani ili iwe imani inayoweza kukusaidia.
Lakini kama huna neno la kutosha ndani yako utaishia tu kujijengea imani kwamba Mungu anaweza na imani yako itakuponya lakini nakuambia imani pasipo matendo hiyo siyo imani.

KWA JINA LA YESU KRISTO MUNGU AKUFUNGUE FAHAMU ZAKO UJIJUE KWAMBA UKO MAHALI GANI NA NEEMA YA WOKOVU IKAKUFUNIKE MAANA BILA WOKOVU IMANI YAKO YA KWAMBA UNA YESU AU MUNGU ATAKUTENDEA NI IMANI HEWE MAANA HAINA MATENDO.

#Powered_By_Holly_Spirit


IN ENGLISH


PRACTICAL IN THE NAME OF JESUS ​​CHRIST

Glory and glory are to JESUS ​​CHRIST who gave up the permit and made it an ideal time for learning his Word again.
We stand against every enemy plan to blind the minds of the people to understand this lesson and to eliminate every thought to obey Christ from now on.
IN THE NAME OF JESUS ​​CHRIST
AMEN

Today we study a lesson with the theme,

THE NAME OF FAITH SHOULD HELP YOU

The purpose of the Holy Spirit to teach us this lesson is to help you realize that no matter how great faith you may be, it can be a great deal of faith, but you do not understand how your faith is built or built, it will never be helpful. to you.
JESUS ​​IS NOT ASKED.

READING 11: 1
So faith is the surety of things hoped for, the clearness of things that are invisible.

**************
This does not matter what religion you are, or you do not really have religion or no matter who you worship but the meaning of faith is this.

Having such a creed based on certain actions will give you the possibility of what you believe to happen as you have the criteria.

But here I am today talking about the faith in believing in God through His word.
How can we assure ourselves that we have faith that can help us by hearing the word?

JAMES 2:19
You believe that God is one; they do well. The demons also believe and tremble.

****************
The fact is that every sophisticated living creature is absolutely convinced that God is one and is totally incapable of doing anything at any time.
Now there are people saying that they do not need to know more about their beliefs but just believe in them is that God exists.

But what they believe in them and the demons they believe is one thing according to the Scriptures or the word of God.
You believe in God that it is one; you do very well, but you know that your faith is the same as that of the devil again that devil goes on in faith because he believes in him until he is shocked.

Satan believes God is strong and can not even try to contend with him and that is why he directs his anger to us who are God's children.
And God gave us the antichrist that is the name of Jesus through salvation.
And if that name properly uses it, we must overcome him, but now Satan is blinding you because you know that you will have the right to stop him from using that name in Jesus Christ that comes with grace.
You do not have to let your consciousness believe salvation will mean that he will fail and will be very difficult for him.

Now you remain rejecting salvation while using the name of Jesus in your religion that can not give you the authority to use that name.
You keep saying that your faith will heal you.
Faith that helps you is the essence of the Word of God.

TWO OF THE FAITH

FIRST FAITH

LUKE 8: 43-48
And one woman, who had been bleeding for twelve years, [who had been paid all her belongings by giving her physicians] should not be healed by anybody,

she went behind him, and touched the skirt of his garment; and immediately from her blood it ceased.

Jesus said, Who touched me? Then all the people disputed, and Peter said unto him, Master, these multitudes are round about thee, and persecuting thee.

Jesus said, "Someone touched me, for I perceive that power has gone out of me."

When the woman saw that she could not move, she came trembling, fell before him, and told the people why she had touched him, and how she was healed immediately.

He said to Daughter, your faith has healed you; go your way in peace.

**************

This woman had a faith that led her to Jesus Christ after hearing him and following him touched the skirt of his garment.

He believed that Jesus healed but not only believe but there were actions he did until he received the healing that followed him and touched the skirt of his garment.

TWO TIME

MATTHEW 8: 5-10
When he entered Capernaum, an officer came to him,

he begged him, saying, Lord, my servant is lying at home, sick of paralysis, he is very sick.

And Jesus said unto him, I will come, and heal him.

The centurion answered him, saying, Lord, I am not worthy that thou shouldest enter under my roof; but just say the word, and my servant will recover.

For I am a man placed under authority, having soldiers under me; saying to this one, 'Go,' he goes; and this one, Come, come; and my servant, Do this, you do.

When Jesus heard this, he marveled, and said unto them that followed him, Verily, I say unto you, I have not seen such great faith in all Israel.

**************

The centurion believed Jesus and followed him to heal his servant and Jesus wanted to do the same thing, but we see that he had a different belief that even surprised Jesus.
He tells her not to follow her but just say the word and her servant will recover.

Both of these men had faith in Jesus,
But their beliefs were not without works and even their actions are not the same.
One believed Jesus healed but by touching the garment of his garment.
This woman would have had the same faith as that of the captain and would not have touched the dress of the garment but just listened to the word and would have recovered,
Because we see an atheist believed Jesus also cures but even by his word.

LUKE 5:17
And it came to pass in those days, that he was teaching; and there were sitting of the Pharisees and of the scribes sitting in every city of Galilee, and Judaea, and Jerusalem; and the power of the Lord was there to heal.

*****************

Even in the doctrine of the power of God there is only a belief in healing.
Now you say that your faith is healing you simply without any knowledge. Where is your faith based?
You who do not want to be saved and feel yourself trusting in God in what way if you do not want to obey his word saved?
Is your belief just like the devil that you believe God is one and obeys his word?
What difference do you have with the devil?
Satan believes God is one and does not obey his word.
You and you believe God is one and obeys his word and that's why you do not want to be saved.
Are you different from the devil? TIME.

Romans 10:17
So faith, the source is to hear; and hearing comes by the word of Christ.

*************

To begin to have faith you must hear the word of Christ and obey it.
But you claim you hear the word and when you do not know what the word is telling you.

FAITH IS NEED TO GOD'S WORD, HUMAN RESPONSIBILITIES WILL HELP OUTCOMES INFORMATION THAT THE FAITH WILL BE LOST TO LISTEN THE FIRST FIRST NOTE.

You can not just say that your faith will heal you, the faith that can help you is the one that comes by hearing the word of Christ.
Faith in many places but in addition is the belief based on the word of Christ.
And the word of Christ must give you guidance to do some thing so that the faith may be overturned or that word becomes common to you.
There is more to do more than trust in God so that our faith will have more consequences than that of the devil who again believes in God and trembles.

JAMES 2:17
Likewise, faith, except in works, is dead in itself.

******************
When you believe that God blesses you must do certain things according to the Bible that a person wants to succeed must do with believing in God, and these actions are also directed by the word too.
You believe God blesses and achieves you but even how much your faith is to work.

REVELATION 28: 8
The Lord will command the blessing come upon you in your storehouses, and all the things that you will put on your hand; and he shall bless thee in the land which the LORD thy God giveth thee.

******************
In trusting in God you must do the work of your hands so that blessings will pass away.
He said he will bless you and believe but not whether you will dream or will wake up sleep but you must work with your hands.
He will command the blessing come to you in your storehouse, if you do not have the storehouse where will the blessing go?

And besides all, no work of the hands that benefits God's blessing as tithe and sacrifice means what you sow is what you will reap.

HAGAI 1: 9
You're looking for many, though there's just a few; and when you came home, I turned it over. Why? Says the Lord of hosts. It is because of my house that remains a perilous state, when you run every one to his home.

**************
If you are told to contribute to church construction you feel that you benefit the pastor.
That's the result.
Thank you God and you are a requester, you have done the same work as a word that leads to you and you wait for blessings but God says you expected to be blessed but blessed because he did not build his own house.
Now you continue to say that your faith cures you or will help you tell you you will continue to set a fire seat.

HAGAI 1: 6
You sow a lot of seed and reap a little; You are eating but you do not eat. you drink but are not filled with drinks; You wear clothes but no fire; and he who earns wages earns wages to get it into a hired bag.

*****************
You wonder how much you earn a lot but that debt does not last.
You eat well but you have no peace with your diet.
You do not understand the eleven how your money goes, but you find it just gone.
You start cutting off the iron and when the iron is brought it yourself.
Faith that does not lead you to do is an air belief and it does not help you.
Your self-esteem is very conscious of your belief in God and you do not want to be saved by the wind.

God has laid the basis for believing that you must go through Jesus Christ.
Otherwise it is wind blowing.

JOHN 17: 3
And this is eternal life, that they may know thee, the only true God, and Jesus Christ whom thou didst send.

*****************
if you expect life based on it is that.
Knowing or believing only God did not come to pass without knowing Jesus Christ who sent him.
And Jesus says to come to him you must be saved.

Other beliefs can be very serious but no action is free.

I SHOULD BELIEVE THAT YOU LOVE GOD

1-CONTACT US
No one on earth does not say that he loves God.
And he is fully convinced that God is the Almighty.
She feels quite fond of her, but her belief is a spirit and does not like God.
There are things we look at and then read the Bible we see you do not love God anymore.

JAMES 4: 4
You prostitutes, do you not know that being a friend of the world is being an enemy of God? So whoever will be a friend of the world makes himself an enemy of God.

*****************
If you're a prostitute you can not tell me that you love God.
Your faith is air although you believe that you love God.
You love the world and its worthless things you can not be a friend of God.

Romans 12: 1-2
Wherefore, my brethren, I beseech you, by the grace of God, take your bodies a living sacrifice, holy, acceptable to God, which is your earnest service.

And do not follow the way of this world; but be transformed by renewing your motives, so that you may know the good, pleasing, and perfect will of God.

*****************
There is someone you see really dressed in a wonderful dress ananodal hips on the road and on the network but he tells you I'm saved and I love Jesus.
Asking about her disgusting tells you that God will not look for the body.

My brother God looks at all things even in your ways.
You wear a dress that you stand with an unsaved person shows you any difference then you say you're saved.
I tell you you are the one who believes that you are saved but there is no salvation.
God would not be watching the body without saying that we should present our bodies as a living and holy sacrifice.

When you wear a trouser you are a woman who is not self-confident and decides to show you what you guys mean for me and I'm pretty.
You say you love God but you disagree with his writings?

JOHN 14:15
If you love me, you will keep my commandments.

**************
You can not love God and then look for legitimacy to resist even one scripture from the Bible.

You have been told not to keep track of the nature of the world because when you love God you are no longer in this world.
It must be different from those in the world.

I say to those in the world that if you really love God you are far from the world and its things.

JOHN 17:14
I have given them your word; and the world hath hated them; because they are not of the world, even as I am not of the world.

***************
I tell you absolutely if you love God you can not get your body again you'll be ashamed to wear clothes just to show the hips.

It is also amazing to tell a woman about the pants who totally opposes who opposed her word.

DANIEL 3: 20-21
Then he ordered some of his men of war to bind Shadrach, Meshach, and Abednego, and throw them into the fiery furnace.

And they were girded with their robes, and their coats, and their garments, and their garments, and were cast into the midst of the burning furnace.

***************
You say that the Bible does not say that the pants are a man's garment. What are those dressed in this garment?
What do you think about this line?
And it was God himself that decided and created this garment and said to be clothed with the men who are you now to argue?

FROM 28: 42-43
And thou shalt make linen pants for thyself, to cover the nakedness of their flesh; These pants will come from the waist to the pants;

and Aaron and his sons shall put them on, when they come into the tabernacle of the congregation, or when they approach the altar to minister in the holy place; lest they bear iniquity, and die; This shall be an everlasting statute unto him, and to his seed.

*************
If God has said this to be a woman's dress, how do you start dressing?
Here is the belief that you love God without keeping His commandments.
If you decide to be saved and if you can not still wish the world you continue with it.

EPHESIANS 2: 1-3
And you were dead because of your sins and sins;

which you formerly walked by following the natural world, and following the king of power, the spirit who works now in the rebellious sons;

who in the past, all of us and we walked among them, in the desires of our bodies, when we fulfilled the desires of the body and of the mind, became our behavioral children like the other.

***************
If you were evil for those things that the nations worry about how you say you are saved and yet your conduct and actions are the same?

The rebellious children are those who are seduced and still live the same life.
Are you ready to be called a rebel son unless you have such a kid?

2-LOVE AND LOVE

To know that you love God or prove that you love God not merely believing in your heart even though you feel that you have a great deal of faith in it.

1 JOHN 4: 8-9
He who does not love, does not know God, for God is love.

In this love God appeared to us, that God has sent His only begotten Son into the world, that we might gain life through him.

****************
If you do not love then let yourself know that you do not have a God or God who loves you but is simply ignorant and unable to evaluate who you love.

1 JOHN 4:20
If anyone says, 'I love God,' and he hates his brother, he is a liar; For he that loveth not his brother whom he hath seen, can not love God whom he hath not seen.

*****************
The only way to know whether you love God or not is to keep His commandments, including this to love all people.

If there is anyone hating you on earth then it is a statement that you do not love God.

YOUR BENEFITING FAITH THAT YOU LOVE GOD ARE NEED TO IMPLEMENTATE THE PROBLEMS OF THE FIRST PEOPLE.

There should be no one to hate in your heart, or revenge, anger, and other things like that and then convince yourself that you love God.

Also to believe that you love God you must do it yourself.

JOHN 3:16
For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth on him should not perish, but have everlasting life.

***************
The symptom of being aware that you love is devoted,
Commitment for the Lord's work, devoted to those in need of various things.

If you love God you will love people whom you see and love you must do to preach the gospel to them to meet Jesus to save them.

That's why even Jesus said,

MATTHEW 25: 34-40
Then the King will say to those on his right hand, Come, blessed of my Father, inherit the kingdom which has been prepared for you since the foundation of the world;

for I was hungry, and you gave me food; I was thirsty and thirsty; I was a stranger, you welcomed me;

I was naked, you clothed me I was sick, you came to look at me; When I was in prison, you came to me.

And when the righteous answer him, saying, Lord, when did we see thee hungry, and weary thee, or thirsty, and weary thee?

And when did we see you a stranger, welcome you, or naked, wearing you?

When did we see you sick, or in prison, when we came to you?

And the King shall answer, saying, Verily, I say unto you, As ye have done unto one of my least brethren, ye did it unto me.

*****************
If you have money but are yours and do not have any help for the needy to love God for where?
You have wealth until the extra but you do not know anything about your neighbor or relative who needs help then how do you say you love God?
You only convince yourself that you love God but the love for others you see with eyes is no love there for a God who does not see him.

When you convince yourself that you love God you must associate with these actions so that you can be sure of your faith.

MATTHEW 5: 44-48
But I tell you, love your enemies, pray for those who persecute you,

that ye may be sons of your Father who is in heaven; for he makes his sun rise upon the wicked, and sendeth forth rain upon the just and the unjust.

For what reward do you love those who love you? Even tax collectors, do you? And do not they do it?

And if you just hear your brothers, what extra action do you do? Even people of the nations, do you? Do not they do that?

So you will be perfect, just as your heavenly Father is perfect.

*****************

The difference between you and the Gentiles will be when people see you fearful and trembling and boasting themselves with their mouths that you really are a child of God or really you love God.

It is very difficult for a Gentile to love his enemies and to pray for him,
If your faith tells you that you love God, then God must be in you and His Spirit will love the one who made you sin even as he began to love us while we were still wrong with Him even sending His Only Son to reconcile us by removing the prosecution for himself so that we could to draw close to him.

A person who does not love God hates his enemy but you who believe that you love God should show yourself in actions to be different from him because the God in you is not partial.
If you see that failure then get yourself aware of it is a sign of love for God and not in you.
In order to become a son of God you must love all people as God himself because he has been in you as his son.
Otherwise you will be giving the free faith that you love God.
The sign of love for God is to be perfect and to have all the qualities God has for you to be with him in one place.

Your faith should be accompanied by actions to make sure that what you believe is yes or not.

Image

1 PETER 3: 7-9
Likewise, ye husbands, abide with your wives in mind; and to give her the honorable wife, as a weaker vessel; and as joint heirs of the grace of life, that your supplication may not be hindered.

The last word is this; one minded, forgiving one another, having brotherly affection, tenderly compassionate, lowly in heart;

people who do not pay bad for bad, or for compost; but blessed are they; because that is what you were called to inherit the blessing.

****************

You may have the greatest confidence that you will be blessed with you and your family, who you and your wife or you and your children and your husband.
But in order for those beneficiaries to have blessings there are things that you should do in the very least that are the ones mentioned here.
If you believe in blessing and then honor your wife, know that your faith is free, so your prayer will be restrained.

You must have one mind, compassionate and loving one another with humility, not covetously wrong with one another, but one who blesses the evil and does not blame it, and then you will have strong faith that the rewarder will be blessed.
And the blessing is also that the successor will still have to do as to work, to give tithes and offerings as what a person wants to do, will build the house of the Lord as we have seen above as well as devoted ourselves to God.
If you do all of this then you will have the confidence that you will be blessed, but otherwise your faith does not have any works that are dead.

Another example is that a person who believes that he or she will have a good partner in life is the one who first started to be good to get the same as the biblical text says God gives you the same as you.
Now you continue to convince yourself that you will find someone who is intelligent if you are zero.

COLOSSIANS 3:16
Let the word of Christ abide in you in all wisdom, in teaching with psalms and hymns, and in spiritual songs; while singing God with grace in your hearts.

***************

When the word of Christ abides in you, you will realize that whatever your faith requires you to do is to be a faith that can help you.
But if you do not have enough word in it you will just stop building the belief that God can and your faith will heal you but tell you faith without doing so is not faith.

FOR THE NAME OF JESUS ​​CHRIST GOD THINK YOURSELF THAT YOURSELVES THE WORD OF THE WORDS OF THE WICKED WILL NEED YOU THE WORDS TO THE WICKED YOUR BELIEVE THAT YOU ARE JESUS ​​WHEN GOD WILL LOVE YOU YOUR LOVE HUMAN RIGHTEOUSNESS.

#Powered_By_Holly_Spirit

No comments:

Post a Comment