Monday 15 October 2018

UNAMAANISHA NINI UNAPOSEMA UNAMSIKILIZA MUNGU WALA SI MWANADAMU?

BWANA YESU APEWE SIFA NA UTUKUFU WOTE

UNAMAANISHA NINI UNAPOSEMA UNAMSIKILIZA MUNGU WALA SI MWANADAMU?

Hicho ndicho kichwa cha somo tunaloenda kujifunza tena leo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Lengo la somo letu ni kudhamiria kuangalia kwamba ni kwa jinsi gani tunavyoweza kumsikiliza Mungu katika kila jambo na kuacha kweli kuwasikiliza wanadamu ambao mara zote maneno yao yanakuwa ni kwa lengo la kupindisha tu hatima yako Mungu aliyoiweka ndani yako.

Kwanza kabisa tunamwangalia mwanadamu ni nani kibiblia,

MWANZO 6:2
wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

*****************

Walio wa Mungu ni wale anaowaita wana, ambao hili neno linatuambia kwamba hao wana waliwaona binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri wakajitwalia wawe wake zao kitu ambacho hakikumpendeza Mungu yani walio wana wa kwake kuoana na binti za wanadamu.
Mwanadamu hajawa mwema kabisa kwa Mungu na hili neno mwanadamu linaanza kutumika hapa katika biblia tukianza kusoma kutoka MWAZO SURA YA KWANZA MSTARI WA KWANZA na katika hili neno kuanza kutumika hapa aliyeitwa mwanadamu ameonekana kuwa na mambo yasiyompendeza Mungu.

YOHANA 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

***************
Kwasabubu basi Mungu aliupenda ulimwengu aliona atoe kitu chenye thamani sana ili kimkomboe huyo mwanadamu ambaye alikuwa kinyume na mpango wake.
Alimtoa MWANA ambaye ni mpango wake ili akamfanye huyo mwanadamu kuwa MWANA yani wawe kitu kimoja maana sisi tuliofanyika kuwa wana wa Mungu ni mwili wa Kristo.
Hivyo mpango wa Mungu ulikuwa sisi sote tuwe wana au watoto wake walio wa thamani mbele zake na ndiyo maana akamtoa mwanawe na sisi tulio okoka tukafanyika kuwa wana kutoka kuwa wanadamu.

MWANZO 6:4
Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile;tena ,baada ya hayo ,wana wa Mungu walipoingia kwa binti za binadamu,wakazaa nao wana;hao ndiyo waliokuwa watu hodari zamani ,watu wenye sifa.

*****************
Wale ambao angalau Mungu aliwaona ni wakwake walianza kuchangamana na wanadamu wakawa chukizo kwa Mungu.

Wana wa Mungu waliingia kwa binti za wanadamu wakazaa nao wana.
Unaona hapa kwamba binti za wanadamu wamezaa na wana wa Mungu lakini kilichozaliwa kinaitwa mwana maana hicho kilichozaliwa kwa dhambi Mungu hakukihesabia dhambi.

MATHAYO 17:5
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.

***************
Tunaona mara nyingi wakati Yesu akienda kuomba alikuwa anaongozana na Petro na wakati wakiwa katika kuomba Mungu akawathibitishia kwa sauti kutoka mbinguni kwamba wamsikilize Yesu ndiye mwanawe mpendwa aliyependezwa naye.
Siyo mtu wake, wala siyo mwanadamu wake bali ni mwanaye.
Hivyo mwana ni yule aliye mpendeza Mungu na tunapaswa kumsikiliza lakini mwanadamu hunena yaliyo yake.

Neno la msingi katika mafundisho yetu ni kutoka

MATENDO YA MITUME 5:29
Petro na mitume wakajibu, wakisema, Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.

*****************
Makuhani waliwakataza wanafunzi wa Yesu wasilihubiri tena jina la Yesu lakini Petro akawajibu kwamba hawataweza kumtii mwanadamu.

Petro aliwaambia hivyo kwasababu hao makuhani walikuwa wanawaambia wasifanye ambacho Mungu alitaka wakifanye.
Tukumbuke kwamba Yesu aliwaambia walihubiri neno lake.

LUKA 24:46-47
Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

***************
Sasa hapo Petro alitambua kwamba wanamkataza kitu ambacho Yesu aliwaelekeza na ndiyo maana akawataja kwamba ni wanadamu kwakuwa walichokuwa wanamwelekeza hakitokani na neno la Mungu.

Lakini tambua kwamba anayekueleza habari zilizo ni mapenzi ya Mungu wewe kuzijuwa hupaswi kumpuuza.
Yako mambo mengi sana ambayo hatuyajui wala hayajaandikwa kwenye biblia na ndiyo maana Yesu alisema hivi,

YOHANA 16:12-13
Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa.

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake.

******************
Yesu anakiri kwamba yapo mengi hatukuelezwa naye yani neno halijasema na ukifungua biblia huwezi kuyakuta yameandikwa.

Roho mtakatifu ndiye anayetufunulia na yuko ndani yetu anaongea hanyamazi kabisa kwa habari ya kutaka mtu ayafuate yote yaliyo mapenzi ya Mungu.

Kama kweli umeokoka na unaongozwa na Roho kuna mavazi ambayo ukivaa tu Roho inakuambia acha mavazi haya japo biblia haiyazungumzii lakini Roho mtakatifu yupo.
Kuna namna tu ukitaka kunyoa nywele zako kwa namna fulani utasikia ndani yako sauti inakuambia wewe uliye mwana wa Mungu hustahili kunyoa namna hii.

Hivyo ni lazima kabisa uambiwe ukweli japo utakuwa mbishi ila sisi watumishi wa Mungu na Roho mtakatifu aliye ndani yetu haturuhusu sisi kukuacha na njia zako mbaya.

Yapo mambo machache sana hayajathibitishwa kabisa kwenye biblia kutokana na nyakati lakini Roho wa Bwana yupo anatufundisha na kutushughudia ndani ya dhamira zetu kwamba si halali kufanyika kwa mtu aliye okoka.
Sasa ni lazima utaambiwa ukweli uiache hiyo tabia.

EZEKIELI 33:8-9
Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la     kumwonya mtu huyo, aiache njia yake, mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini     damu yake nitaitaka mkononi mwako.

Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye     asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.

*****************
Unapokuwa ni mwana wa Mungu ujue kabisa huwa Baba anakuambia mambo mengi sana kupitia Roho wake na ndiyo maana Yesu anasema

YOHANA 14:10
Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Hayo maneno niwaambiayo mimi siyasemi kwa shauri langu; lakini Baba akaaye ndani yangu huzifanya kazi zake.

**************
Huwa Mungu hamfichi mwana jambo lolote atakuambia,
Jinsi ulivyo mwana wa Mungu basi wewe kila utakachokiongea si kwa shauri lako na ndiyo maana Mungu anasema nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo aiache njia yake basi akifa wewe utadaiwa.

Wewe uliyefanyika kuwa mwana wa Mungu ni sauti ya Mungu kabisa.

Wewe unayeambiwa au kuonywa jambo na sauti ya Mungu lakini unaendelea na kusema eti humsikilizi mwanadamu na unaendelea basi ujue kabisa hujui unachokifanya.
Unatakiwa utubu na kuacha kiburi.

Halafu wana wa Mungu hawanyamazi kwakuwa wanaye Roho anasema ndani yao wala si wao wenyewe halafu wewe unayepuuza ndiye mwanadamu ila hujitambui.

Ukiambiwa ukweli unabaki kusema usihukumu usije ukahukumiwa.
Ingekuwa na hivyo kusingekuwa na kuonyana. Sasa elewa maana halisi ya andiko hili.

MATHAYO 7:1-5
Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi.

Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.

Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?

Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.

******************
Hakuna mwanadamu anayepaswa kuhukumu ila mwana wa Mungu anahukumu zote.
Huwezi kumwambia nduguyo ngoja nitoa kibanzi ndani ya jicho lako kumbe mna boriti ndani ya jicho lako.

Boriti ni kitu kidogo sana kuliko kibanzi, Yesu alitumia mfano huu kwasababu alitaka kuwaelekeza wale wanao hukumu wasihukumu kwa kuwaangalia wengine kwakuwa wamekosa bali na wao pia wajiangalie je wako sawa?

Kama anayehukumu mtu aliyezini basi asije akawa yeye anasengenya au kuna dhambi ya siri yoyote anayoifanya.
Sasa tunaona namna ambavyo Yesu anaendelea kusema kwamba itoe kwanza ile boriti ndani yako.
Na ukishaitoa basi unaruhusiwa kukitoa kile kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
Ndipo utakavyoweza kukiona vyema kibanzi kwenye jicho la nduguyo.
Kwa maana nyingine ni kwamba ukiwa msafi unaweza kuutumia usafi wako kisha ukajilinganisha na mtu mchafu na ukauona uchafu wake.

Unapokuwa mwana wa Mungu yani mtakatifu wewe unaweza kabisa kumwambia mtu hatima yake kutokana na mwenendo wake na ikawa hivyo.
Kama mimi naliishi neno kwa asilimia mia moja halafu nikakuona wewe unaishi tofauti na mimi basi mimi naweza kukuambia ukweli kwamba wewe utaenda motoni na kama hutaki kuamini kwamba si mimi niliyesema bali ni Mungu wewe acha kutubu na kubadili hiyo dhambi niliokuhukumia nao halafu ufe hivyo hivyo tuone kama hutaenda motoni kweli.

WAEBRANIA 4:12-13
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.

*******************
Neno la Mungu linachoma kweli na ndiyo maana mtu mwenye hilo neno akikuambia ukweli mapepo yaliyo ndani yako yanalipuka unajikuta unaanza kutukana na kukasirika yani unaendelea kujipigilia msumari.
Yani unapenda injili za kutiana moyo lakini hutaki kuambiwa ukweli.

Hakuna kiumbe kisicho wazi na kuwa utupu juu ya neno la Mungu.
Kama nimejaza neno la Mungu ndani yangu halafu nikakutazama wewe na mwenendo wako kisha nikakulinganisha na neno huwa nakutambua kabisa kwamba wewe ni mwovu, hujaokoka wala huna sifa za kujiita mlokole labda ubadilike na ujue kabisa hapo siongei mimi bali neno la Mungu ndilo linaloongea.
Nitakushangaa unapokuwa unasema eti humsikilizi mwanadamu.

YEREMIA 1:9
Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;

********************
Fikiri huyu huyu Yeremia kuna watu walikuwa wanampuuza wakati akiwafikishia unabii.
Lakini ukweli alikuwa anaongea maneno ya Mungu na ni sauti ya Mungu.
Ni mara ngapi wewe umekuwa unapuuza maneno ambayo Roho mtakatifu amewaagiza watumishi wa Mungu wakufikishie ukaishia kusema simsikilizi mwanadamu?

Watu wanataka wafundishwe jinsi wanavyotaka wao bali si kile wanachopaswa kufundishwa.
Yani mtumishi wa Mungu anakufundisha lakini badala ya kumtii Mungu unajikuta wewe unaanza kumfundisha.
Unajiona unajuwa kila kitu lakini ukweli ni kwamba hujui kitu chochote hapa duniani yani kwa kifupi hujijui hata wewe ni nani.
NAKUONEA HURUMA SANA.

HUFUNDISHIKI YANI HUJUI NA HUJUI KAMA HUJUI KITU CHOCHOTE.

Mtu kaja kukufundisha unamdharau na kuchukua tu andiko moja ukalitafasiri jinsi unavyotaka wewe ili liendane na dhambi yako halafu unasema eti humsikilizi mwanadamu bali unamsikiliza Mungu.

Yani ukisoma mstari kwenye biblia huna haja ya kuuchambua na kugundua Mungu anasema nini na wewe bali unaanza kujiuliza kwamba dini yako inasemaje kuhusu huo mstari na ukiuona uko kinyume na dini au matendo yako basi unauweka pembeni haukufai.
Huyo Mungu sijui unamsikiliza kwa njia gani.
Wengine mnadhiriki hata kusema mchungaji kitu gani mimi mchungaji wangu ni Yesu, are you serious???????????

YEREMIA 3:15
nami nitawapa ninyi wachungaji wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha kwa maarifa na fahamu.

*****************
Yesu ni mchungaji wetu sawa, lakini siyo kwa namna unayoiongelea wewe ili uharishe tu na kinywa hicho hicho unachokitumia kupinga nacho neno lake baadae unamwomba nacho Mungu na unajihesabia haki wala hutaki kutubu na kuacha.

Mchungaji wako ndiye amepewa huo ufahamu wa kukuelekeza njia ya kwenda kwa Yesu hivyo unatakiwa kuwa mtii na kunyenyekea na ndiyo maana atakuja kutoa hesabu yako mbele za Baba.

YOHANA 17:12
Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.

***************
Kwa kupitia jina la Yesu na neno lake mchungaji anakuongoza wewe lakini kwakuwa tu una vijisenti vyako unajidanganya kwamba humsikilizi mwanadamu.

Mwanadamu ni pale anaposema maneno yake pasipo kuongozwa na Roho lakini anapokufundisha kwa kupitia neno la Mungu basi hiyo ni sauti ya Mungu na kama usipotii dunia itakunyoosha tu.

MATHAYO 28:18-20
Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

******************
Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba wakaihubiri injili kwa jina lake,
Alipokuwa nao walikuwa wanafunzi lakini alipoondoka tu wakafanyika waalimu wa kuwafundisha mataifa yale aliyowafundisha wao na wakaanza kuitwa wakristo.

Watu wanajiita wakristo lakini ni wapinga Kristo wakubwa.
Ukitaka kujiita mkristo ni lazima utii yale yake yote na ulifuate neno lake lote maana anasema kuwa mkinipenda mtazishika amri zangu.

Kama sisi tumetumwa kuwafanya kuwa wanafunzi inamaana unatakiwa unapoelekezwa jambo la Kristo basi uwe mwanafunzi ukae chini uwe na utayari wa kufundishwa na siyo wewe ujitutumue tena na kujifanya unataka kumfundisha huyo anayetaka kukufundisha wewe.

MARKO 16:15-16
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

**************
Tunamuona tena Marko anaongea kile kile ambacho Mathayo alichokiongea, wote walisikia maneno hayo ya mwisho aliyoyaongea Yesu wakati akiwaaga moja kwa moja.
Kuambiwa ukweli wewe ni lazima ili uokoke.

WARUMI 10:13-14
kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.

Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri?

******************
Ni haja ya Bwana Yesu kila mtu aliitie jina lake ndiyo maana akatutuma sisi kulihubiri neno lake katika kweli yote.
Lakini wewe unafikiri ni mwanadamu anaongea na wewe.

LUKA 24:46-51
Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.

Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki.

Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni.

*******************
Kama mataifa yote yatahubiriwa kwa jina lake wewe unafikiri ni nani atakayehubiri kama unapoambiwa ukweli unasema ni mwanadamu?

YOHANA 20:22-23
Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.

Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

***************

2 WAKORINTHO 13:1
Hii ndiyo mara ya tatu ya mimi kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.

******************
Turejee kidogo kuanzia Mathayo hapo juu halafu umsome Marko kisha umsome Luka umalizie na Yohana.

Hawa wote wameandika maneno ya Bwana Yesu ya Mwisho kabisa kuongea nao ana kwa ana ndipo akaondoka.
Wote wameyaandika lakini kila mmoja aliandika kwa namna yake ila hakutoka kwenye lengo la Yesu na kati yao wote hatujui ni yapi ambayo Yesu aliyatamka kama yalivyoandikwa ila wote ukiwasoma wanalenga kitu kimoja.

MFANO
Tunaweza tukawa tumeketi watu watatu mahali pamoja halafu mimi nikaondoka nikasema
"NAENDA CHOONI NARUDI SASA HIVI"
kisha nikawaacha nyie wawili.

Halafu baada ya muda kidogo akaja mtu kuniulizia,
Mmoja anaweza akamjibu kwamba
"AMEENDA KUJISAIDIA ANARUDI SASA HIVI"
na mwingine akamjibu
"AMEENDA UWANI ANARUDI SASAHIVI"
Lakini ukweli ni kwamba mimi sikutamka neno hata moja kati ya hayo waliyoyatamka lakini wote waliotamka hawajatoka nje kabisa ya kuelezea nilikoenda.

Lengo la Yesu kuja duniani ni ili watu wakombolewa kutoka kwenye dhambi,

TWENDE TARATIBU KWA WALE WANAOAMBIWA UKWELI KWAMBA TUSITUBU KWA WATU LAKINI WANAKUWA NA KIBURI KUFUNDISHWA.

MATHAYO 28:19-20
Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

***************
Utakapokubali kuwa mwanafunzi na ukawa tayari kufundishwa ni lazima utamjuwa Yesu na utamkiri na kukubali kuwa una dhambi, utaokoka na utabatizwa na kuwa mkristo kamili.

MARKO 16:15-16
Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.

*****************
Hawa wanafunzi wa Yesu watakapoihubiri injili watakaoamini ile injili wataokoka na kubatizwa na mwisho hawatahukumiwa na dhambi maana watakuwa wameshasamehewa.

LUKA 24:46-48
Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu;

na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu.

Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.

******************

Mataifa watakapohubiriwa habari zake kwa jina lake watakapozikubali hizo habari za toba wataondolewa dhambi nao wataokoka na kuurithi uzima wa milele.

YOHANA 20:22-23
Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.

Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

****************
Hapa ndiko panapowachanganya wale wanaoenda kuungama na kutubu dhambi kwa watu wakidhani wana mamlaka hiyo.

Huyu Yohana aliandika kwa kifupi sana lakini bado hakutoka nje ya malengo ya uandishi wa hao wengine.

ALIMAANISHA HIVI
WOWOTE MTAKAOWAONDOLEA DHAMBI WAMEONDOLEWA NA WOWOTE MTAKAOWAFUNGIA DHAMBI WAMEFUNGIWA_____Mimi nilikaa nanyi na kuwafundisha kila kitu na nyie ndiyo mnaoujua ukweli wote kwamba mtu akinipokea mimi ataondolewa dhambi, kama mkinitii na mkaenda kuwahubiria habari njema juu yangu basi watanijuwa mimi na wataokoka na kuondolewa dhambi zao,
Lakini mkiamua mkae tu bila kwenda kunitangaza kwao basi hawatanijuwa na wala hawataokoka wala kusamehewa dhambi hivyo mtakuwa mmewafungia dhambi zao kwamaana hamjawapa neno langu ili wanipokee wasamehewe.

Sasa nikuulize wewe unayekataa kabisa injili na kujiona uko sahihi eti huambiwi kitu na mwanadamu bali unamsikiliza Mungu unaweza ukaniambia unamsikilizaje huyo Mungu?
Au huwa unasikia sauti kutoka mbinguni?

Ni kitu gani kinakupa kiburi kiasi hata cha kumpuuzia mtu anayejitolea kukufundisha bure wala humlipi?

Unasema unaisubiri neema.

TITO 2:11
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa;

****************
MAANA YA NEEMA ni upendeleo, kustahilishwa usichostahili kabisa.
Ni neema ipi unayoitaka wewe zaidi ya ile ya mtu kutumia muda wake akaacha kazi zake ili akuhubirie wewe uende mbinguni?
Kuna mshahara unaomlipa?
Unadhani unastahili hiyo haki ya mtu kuacha kazi zake na kuja kwenye ofisi yako kukuhubiria huku wewe unaingiza fedha?

KUNA KIBURI KINAKUSUMBUA

EZEKIELI 28:17
Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu     ya mwangaza wako; nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama.

****************
Kinachokutia kiburi Mungu anakijuwa na usijidanganye kabisa kwamba Mungu atataka upite njia A halafu wewe ulazimishe kupita njia B na ubaki kuwa salama.

MITHALI 16:25
Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti.

******************

Kwa akili zako za kibinadamu unajiona uko sahihi sana lakini hata ufanye nini na chema kiasi gani bado huwezi kuziona mbingu kama hujaokoka huo ndiyo ukweli.

1 SAMWELI 8:7-9
Bwana akamwambia Samweli, Isikilize sauti ya watu hawa katika kila neno watakalokuambia; kwa maana hawakukukataa wewe, bali wamenikataa mimi, ili nisiwe mfalme juu yao.

Kwa kadiri ya matendo yote waliyonitenda tokea siku ile nilipowatoa katika Misri hata leo, kwa kuniacha mimi, na kwa kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokutenda wewe.

Basi sasa, isikilize sauti yao; walakini, uwaonye sana, na kuwaonyesha desturi ya mfalme atakayewamiliki.

***************

Huyo mtumishi anayehubiri kwenye redio, majukwaani, na wengine kukufuata mpaka uliko lakini wewe kwa kiburi chako unamtolea maneno ya kiburi ujijuwe kabisa na uwe na uhakika humjibu yeye bali ni Mungu.

Sisi tunaelekezwa na Mungu tukuambie ukweli kwamba njia uliyo nayo itakufikisha wapi.
Utabaki ukisema humsikilizi mwanadamu lakini nakuambia hii ni sauti ya Mungu na kama usipo okoka na kumtii Mungu kupitia watumishi wake hutafika popote.

MITHALI 18:12
Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna; Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

*******************
Mtu yeyote aliyetangulia kuwa mtii na kukubali kufundishwa na kutafakari bila kupuuza aliokoka,
Lakini ukitanguliza majivuno na ukijiona tu unajiinua ujue habari yako imekwisha na unaenda kuanguka.

1 YOHANA 2:16
Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

********************
Achana na hii dunia umtii Mungu, uogope dhambi ni lazima utafanikiwa, usijifanye mjuwaji hujui chochote wewe kaa utulie ufundishwe na kadiri unavyokuwa mtii utajifunza mengi na Mungu huwainua wanyenyekevu.

Tamaa ya mwili ni pamoja na mavazi yasiyo na utukufu wa Mungu, mwili unapenda kujionyesha ukoje, na macho hushabikia kila kilichotiwa nakshinakshi na shetani na kiburi cha uzima,
Wewe uliye mzima na kujiona handsome/mrembo kwamba wewe huwezi kuokoka na kuacha starehe basi uwe tu na uhakika kwamba umeshaoza.

1 TIMOTHEO 5:6
Bali, yeye asiyejizuia nafsi yake amekufa ingawa yu hai.

**************
Unajiona mzuri sawa lakini bila Yesu dada wewe umeshaoza, Wewe mwanaume unayejiona unaenda na wakati yani wanawake wewe, pombe na starehe za kishamba uwe na uhakika kwamba umeshaoza.
Wasiyomjua Mungu utawababaisha sana lakini nyinyi nyote ni marehemu mnaotembea.

Watu wanaishi maisha yasiyo yao leo kwasababu tu walijiinua,
Wewe unaye endelea kujiona unajuwa endelea lakini kufa kwako kutadhihirika hivi punde maana ulishakufa.

MUNGU AKUBARIKI SANA

#Powered_By_Holly_Spirit

IN ENGLISH

THE LORD JESUS ​​PROVISES ALL THE FATHER AND THE FULL

WHAT DO YOU MAKE MEANING WHAT YOU SHOULD YOU SHOULD HELP GOD NOT BE A MAN?

That's the subject of the lesson we are going to learn today with the power of the Holy Spirit.

The purpose of our lesson is to focus on how we can listen to God in every matter and to stop listening to people who always say their words are merely aimed at realizing your future God has put in you.

First of all, we look at the person who is biblical,

ACTS 6: 2
The sons of God saw the daughters of men to be good; They took care of all their chosen ones.

*****************

God's people are those whom he calls children, who this word tells us that they have seen the daughters of men as good and self-assuming their own things that displeased God who have his own intimate relations with the daughters of men.
Man is not very good to God and this human word begins to be used here in the Bible as we begin to read from ACTIVITY CHAPTER ONE FIRST STORY and in this word to begin to be used here called a man who has been considered to be displeasing to God.

JOHN 3:16
For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believeth on him should not perish, but have everlasting life.

***************
Sadly, God loved the world he had given something very valuable to redeem that man who was against his plan.
He gave the Son who is His plan to make that human being the ONE CHILDREN to be one thing because we have become children of God is the body of Christ.
So God's plan was for us all to have His precious children or children in His presence and that is why he gave His son and us we are circumcised and made to be humans from human beings.

ACTS 6: 4
And the Nephilim were in the earth in those days: and after that, when the sons of God came in unto the daughters of men, they bare children: these were the mighty men of valor, the men of valor.

*****************
Those who at least God saw them were his men who began to associate with humans and became disgusting to God.

The sons of God came in to the daughters of men who were born to them.
You see here that the daughters of men have begotten sons of God but the birth is called a son because that which was born of sin did not imply sin.

MATTHEW 17: 5
While he was yet speaking, behold, a white cloud cast them forth; And lo, a voice came out of the cloud, saying, This is my Son, my beloved, in whom I am well pleased; listen to him.

***************
We see many times when Jesus was going to pray he was accompanying Peter and while praying to God and vindicated them from heaven to listen to Jesus as his beloved son.
It's not his person, not his human being but his son.
So the son is the one who is pleasing to God and we should listen to him but the man speaks of it.

The key word in our teaching is from

MARKS 5:29
Peter and the apostles answered, saying, We ought to obey God rather than men.

*****************
The priests prohibited Jesus' disciples from preaching the name of Jesus but Peter answered that they would not be able to obey the man.

Peter told them so because the priests were telling them not to do what God wanted them to do.
Let us remember that Jesus told them to preach his word.

LUKE 24: 46-47
And he said unto them, Thus it is written, that the Christ shall suffer and rise on the third day;

and that all nations shall be preached in his name of repentance and remission of sins, beginning from Jerusalem.

***************
Now Peter realized that they were rejecting what Jesus was directing to them and that's why He referred to them as human beings as they were turning their backs on the word of God.

But realize that the one who tells you the information that is God's will you should be aware of should not be ignored.
Your very many things we do not know or are not written in the Bible and that's why Jesus said,

JOHN 16: 12-13
Even though I still have much to tell, but you can not stand it right now.

But when he comes, the Spirit of truth, He will guide them to all the truth; for he will not speak of his own counsel; but whatsoever he shall hear, that he shall speak; and the things which he shall speak shall he tell them.

******************
Jesus acknowledges that there is much that we have not been told by what the word has not said and when you open the Bible you can not find it written.

The Holy Spirit is the One who reveals us and is in us who speaks and does not completely know what to expect anyone to follow God's will.

If you are truly saved and led by the Spirit there is only a garment that you wear on the Spirit tells you to put on this dress even though the Bible does not speak but the Holy Spirit is there.
Just as you want to shave your hair somehow you'll get in your voice that tells you who you are a son of God deserve to shave like this.

So it's absolutely necessary to be told the truth even though you will be a refuge unless we are God's servants and the Holy Spirit within us will not allow us to abandon you and your bad ways.

Even a few things have not been thoroughly confirmed in the Bible from time to time but the Spirit of the Lord is teaching us and dealing with us in our minds that it is not lawful for a person who is envy.
Now you must be told the truth and leave that character.

EZEKIEL 33: 8-9
I say to a wicked man, O wicked man, thou shalt surely die; and thou speakest not to destroy the man, and to leave his way, that wicked man shall die in his iniquity; but his blood will I require in thy hand.

But if you warn someone bad because of his way, the purpose is to stop; neither let him alone; He will die in his iniquity, but you have saved your soul.

*****************
When you are a son of God, know exactly what the Father tells you so much about His Spirit and that's why Jesus says

JOHN 14:10
Do you not believe that I am in the Father, and the Father is in me? The words that I speak unto you I speak not of my counsel; but the Father that abideth in me doeth his works.

**************
If God does not care for anything, he will tell you,
How you are the Son of God, then, whatever you say to yourself is not in your mind and that's why God says I have said to a bad person, O bad man, you will surely die, and you do not say the word to warn the man to leave his way and then die you will be condemned.

You who became the Son of God is the voice of God altogether.

You who are told or told by the voice of God but keep on saying that they do not listen to man and you keep going to know you really do not know what you are doing.
You have to repent and stop arrogance.

Then the children of God do not ignore that the Spirit says in them and not their own, then you who ignore it are human but you do not realize it.

If you are told the truth you are still saying that you should not judge unless you are judged.
It would have been so there would be no cats. Now understand the meaning of this text.

MATTHEW 7: 1-5
Do not judge, lest you be judged.

For the judgment which thou judgeest, that thou shalt be judged; and what measure you are measuring out, that is what you will be exhausted.

Why, then, do you look at the hollows that are in your brother's eye, and not the beam that is within your own eye?

Or how will you say to his brother, Let me take a napkin out of your own eye; and no! Do you have a beam in your own eye?

You hypocrites, first put the beam in your own eye; and then you will find it good to give out the speck in the eye of your brother.

******************
No human should judge except the Son of God judges all.
You can not tell the brother if I give a blanket inside your eye or you have a beam inside your eye.

The beam is a bit smaller than a bucket, but Jesus used this illustration because he wanted to guide those who do not judge by looking at others because they are wrong but they also think they are right.

As a judge of a murderer then let him not be he who slanders or there is any sin of any secret he does.
Now we see how Jesus goes on saying that he should put the beam first in you.
And if you give it then you are allowed to give what you see in your friend's eye.
And you will be able to get a good look at the brother's eye.
In other words, being clean you can use your hygiene and compare yourself to the unclean person and see his dirt.

When you become the Son of God who is holy you can completely tell someone the fate of his behavior and it did.
If I lived a word for one hundred percent then I saw you living differently with me then I can tell you the truth that you are going to hell and if you do not want to believe that I was not the one who said but God would not repent and change the sin I committed to you and then die like you will not go in the fire really.

READING 4: 12-13
For the Word of God is alive, and is sharper, and sharper than any two-edged sword, and is sharper even to divide the soul and the soul, with the joints and the fat that is in it; it is also easier to discern the thoughts and intentions of the heart.

And there is no creature that is not clear before him, but all things are naked and openly exposed to him who has our things.

*******************
The word of God is true and that's why the person with the word tells you the truth that the demons inside you are bothering you find yourself getting scorned and angry as you keep wagging yourself nail.
What do you like the gospel to encourage but you do not want to be told the truth.

There is no invisible creature and being void on the word of God.
If I have filled the Word of God with myself then I have seen you and your behavior then compared you with the word I really realize that you are evil, you are not saved and you do not have the reputation of calling yourself a goddess maybe to change and know exactly where I do not say but the word of God is what it speaks.
I'll be surprised when you say that they do not listen to man.

JEREMIAH 1: 9
And the Lord stretched forth his hand, and touched my mouth; And the Lord said unto me, Behold, I have put my words in thy mouth;

*******************
Think of this Jeremiah that people were ignoring him while prophesying to them.
But the truth was speaking the words of God and it was God's voice.
How often have you ignored the words that the Holy Spirit has commanded God's servants to reach you and end up saying you do not listen to man?

People want to be taught how they want them but not what they should be taught.
Be a servant of God who teaches you but instead of obeying God you find yourself beginning to teach him.
You see yourself aware of everything but the fact is that you do not know anything on earth who simply does not know who you are.
YOU CAN LOOK LIKE.

WHAT IS PREPARATION AND EVALUATION AS TREATED ONLY.

Someone who teaches you is disregarding and just taking one text to interpret how you want it to fit in with your sin and then say that it does not listen to man but you listen to God.

When you read the verse in the Bible you do not need to analyze it and find out what God is saying to you but you begin to wonder how your religion says about that verse and if you see it contrary to your religion or actions then you put it in perspective you did not deserve it.
That God I do not know how you listen to him.
Others are even involved in saying the pastor what is my pastor is Jesus, are you serious ??

JEREMIAH 3:15
and I will give you pastors who love my heart, who will feed them with knowledge and understanding.

*****************
Jesus is our Shepherd the same, but not the way you talk about it to just get hurt with the mouth you use to resist his word later you ask God for it and justify yourself and you do not want to repent and quit.

Your pastor has been given this insight to guide you to the way to Jesus so you have to be obedient and humble and that is why he will come to give your countenance before the Father.

JOHN 17:12
While I was with them, I kept them in your name which you gave me, and I kept them; Not one of them was lost, except the son of perdition, so that the scripture might be fulfilled.

***************
Through Jesus' name and word the pastor guides you but just because you have your pretends that you do not listen to man.

Man is where he speaks his words without being led by the Spirit but when he teaches you through the Word of God then that's the voice of God and if you do not obey the world that will break you.

MATTHEW 28: 18-20
And Jesus came unto them, and spake unto them, and said unto them, All authority has been given me in heaven and on earth.

Go therefore and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost;

and teach them to observe all that I commanded you; and behold, I am with you always, even to the fullness of the dawn.

******************
Jesus told his disciples that they preached the gospel in his name,
When he was with them they were disciples but when he left he was taught teachers of the nations he taught them and became Christians.

People call themselves Christians but they are antichrist.
If you want to call yourself a Christian, you must obey all of it and follow his word. He says that you love me and keep my commandments.

If we are commissioned to make disciples say that you should be guided by Christ and then become a student to be ready to be taught and not to re-introduce ourselves and pretend to want to teach the one who wants to teach you.

Mark 16: 15-16
And he said unto them, Go ye into all the world, and preach the gospel unto every creature.

He that believeth and is baptized shall be saved; he that believeth not, shall be condemned.

**************
When we see him again Mark speaks of what Matthew was talking about, all heard the last words he spoke to Jesus when he slaughtered them directly.
Being told the truth you must be saved.

Romans 10: 13-14
for, Whosoever shall call on the name of the Lord shall be saved.

How then do they look for him who is not a believer? How do they trust him if he has not heard him? How would he feel without a publisher?

******************
It is the need of the Lord Jesus that every one to call his name is why he sent us to preach his word in all truth.
But you think it's a human talking to you.

LUKE 24: 46-51
And he said unto them, Thus it is written, that the Christ shall suffer and rise on the third day;

and that all nations shall be preached in his name of repentance and remission of sins, beginning from Jerusalem.

And you are witnesses of these things.

And, behold, I bring upon you my Father's promise; but stay here in the city, so that you can get the highest strength.

He led them to Bethany, and lifted up his hands, and blessed them.

When it came to blessing them, he separated himself from them; he was taken up to heaven.

*******************
If all nations will be preached in his name, do you think who will preach if you are told the truth you say it's man?

JOHN 20: 22-23
And when he had thus spoken, he rebuked them, and said unto them, Receive ye the Holy Ghost.

Whosoever shall take away sin, they are taken away; and whatsoever ye shall bind on sin, they are bound.

***************

2 CORINTHIANS 13: 1
This is the third time I come to you. At the mouth of two or three witnesses every word will be verified.

******************
Let's go a little bit from Matthew above and read Mark and then read Luke and complete it with John.

All these have written the words of the last Lord Jesus to talk to them and to their children and then left.
They all wrote it but each wrote it in its own form except it did not come from Jesus' goal and among them we all do not know what Jesus said as it was written except all of them read the same thing.

Image
We could set three people together and then I left and said
"I HAVE GOOD REALLY WERE NOW"
then I left two of them.

Then after some time someone came to tell me,
One can answer that
"THEY ARE GOVERNING TO EVERYONE NOW"
and another answered him
"WAYS ARE WERE LOVE"
But the fact is that I did not utter one word among those who spoke out but all the speakers did not come out to tell me where I was going.

The purpose of Jesus to come to earth is for mankind to be redeemed from sin,

Let's go to all those who have been told that the fact that people in the world will have a great deal of confidence.

MATTHEW 28: 19-20
Go therefore and make disciples of all nations, baptizing them in the name of the Father, and of the Son, and of the Holy Ghost;

and teach them to observe all that I commanded you; and behold, I am with you always, even to the fullness of the dawn.

***************
Once you accept being a disciple and are ready to be taught you must know Jesus and confess and acknowledge that you have sin, you will be saved and be baptized and become a full Christian.

Mark 16: 15-16
And he said unto them, Go ye into all the world, and preach the gospel unto every creature.

He that believeth and is baptized shall be saved; he that believeth not, shall be condemned.

*****************
When Jesus' disciples preach the gospel to those who believe the gospel will be saved and baptized and at last they will not be judged by sin because they will be forgiven.

LUKE 24: 46-48
And he said unto them, Thus it is written, that the Christ shall suffer and rise on the third day;

and that all nations shall be preached in his name of repentance and remission of sins, beginning from Jerusalem.

And you are witnesses of these things.

******************

When the nations are preached in his name when they accept the gospel of repentance they will be taken away from sin and they will be saved and inherit eternal life.

JOHN 20: 22-23
And when he had thus spoken, he rebuked them, and said unto them, Receive ye the Holy Ghost.

Whosoever shall take away sin, they are taken away; and whatsoever ye shall bind on sin, they are bound.

****************
Here is where those who go to confess and repent of sin for people think they have that authority.

This John wrote very briefly but did not come out of the goals of the other writers.

THERE HAPPENS
WHO YOU WANT TO DISCIPLE ABOUT OWNERS WHO HAVE BENEFITED BY ALL THAT YOU HAVE FOUND IT THAT YOU HAVE FOUNDED_____I am sitting with you and teaching you everything and you know all the truth that whoever accepts me will be taken away, if you obey me and go preaching the good news about me then they will know me and will be saved and have their sins blotted out,
But if you decide not to go to announce to me then they will not know me and they will not be saved or forgiven of sin so you will have to cover their sins for you have not given my word to receive forgiveness for me.

Now I ask you who reject the gospel and think it's right to say nothing to man but you listen to God you can tell me how to listen to God?
Or do you hear a voice from heaven?

What makes you so proud even to ignore someone who volunteers to teach you free or not?

You say you are waiting for grace.

TITUS 2:11
For the grace of God that saves all men is revealed;

****************
THE NEEMA COURT is a privilege, refinished unworthy.
What grace do you want more than that person's time spent on his work to preach to you in heaven?
Is there a salary that you pay?
Do you think you deserve the right to leave his job and come to your office to preach to you while you're getting money?

THERE IS A BOOK TO REMEMBER

EZEKIELS 28:17
Your heart grew up because of your beauty; you have destroyed your wisdom because of your light; I have thrown you down, I have thrown you in front of kings, that they may look upon you.

****************
What makes you proud of God knows and does not fool yourself that God wants you to go on A path then you have to force the passage B and remain safe.

PROVERBS 16:25
The way seems to be right in the eyes of a person; But the end thereof are the ways of death.

******************

With your human mind you think it is very accurate but what you do and how much you still can not see the heavens if you are not saved that's the truth.

1 SAMUEL 8: 7-9
And the LORD said unto Samuel, Hear the voice of this people in every word that they shall speak unto thee; for they have not rejected thee, but have rejected me, that I should not reign over them.

According to all the works which they have done unto me from the day that I brought them forth out of the land of Egypt unto this day, and forsake me, and served other gods, so do they unto thee.

Now therefore, hear their voice; however, to warn them very much, and to show them the custom of a king who will possess it.

***************

That servant preaches on radio, controversy, and others to follow you until you are in existence but you in your pride give him the words of pride to be completely aware and to be sure he responds to him but to God.

We are guided by God to tell you the truth about where the way you have will bring you.
You will remain saying that you do not listen to man but I tell you that this is God's voice and if you are unwilling and obedient to God through his servants will come anywhere.

PROVERBS 18:12
Before the destruction of the heart of man is haughty; And before honor precedes humility.

*******************
Anyone who was first obedient and accepted to be taught and meditated without ignoring the saved,
But if you start boasting and you just feel up and know that your information is over and you're going to fall.

1 JOHN 2:16
For all that is in the world, the desire of the flesh, and the desire of the eyes, and the pride of life, are not of the Father, but of the world.

*******************
Deal with this world obey God, fear sin must succeed, do not make yourself a nurse you do not know anything you stay so educated and as you listen to learn more and God elevates the humble.

The desires of the body are part of the unfathomable clothing of God, the body desires to be gluttonous, and the eyes are sensitive to everything that is tainted by the devil and the pride of life,
You who are old and feel handsome / beautiful that you can not survive and stop relaxing then be sure that you have lost.

1 TIMOTHY 5: 6
But he who does not restrain himself is dead though he lives.

**************
You feel good as well but without Jesus your sister you have wandered, You are a self-assuming man you are going and when you women, alcohol and comedy pleasures you have to be sure you have wandered.
The ignorant ones will grieve you but you all are late to walk.

People live their lives today because they just got up,
You who continue to see yourself realize you will continue but your death will not appear immediately because you have died.

GOD IS EVANGELIZED

#Powered_By_Holly_Spirit

No comments:

Post a Comment