Tuesday 19 October 2021

USOMAJI WA MAANDIKO

 USOMAJI WA MAANDIKO


Katika usomaji wa maandiko hasa katika vitabu vya manabii, 


Tunapaswa kusoma na kuelewa alichosema nabii kwa ufahamu wake kuhusu wasifu wa Mungu bila usahihi


Si kila mstari ulioandikwa kwenye biblia kuwa ni neno la Mungu


Na si kila alichosema Eliya kumhusu Mungu kwamba alikua sahihi, 


Aliongea kwa kiwango cha ufahamu wake! 


Iko wazi kwamba hakuna mtu yeyote kabla ya Kristo aliyewahi kuwa na Roho wa Mungu ndani yake, 


Roho alikaa ndani ya watu walioamini baada ya ufufuo


Lakini tuangalie hapa


MWANZO 41:38

Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake?


*******


Hayo hapo ni maneno ya Farao kwa mtazamo wake juu ya wasifu wa Mungu


Ni makosa kuusoma huo mstari na kuelewa kwamba Yusufu alikua na Roho wa Mungu ndani yake! 


Wasifu wa Mungu tunaujua kupitia Kristo, alivyokuwa ndivyo Baba alivyo milele yote na hajawahi kubadilika! 


Huwezi kujifunza kumjuwa Mungu kupitia Eliya au Danieli au Ayubu halafu ukabaki salama!


Ufunuo wa Mungu upo ndani ya Kristo


Yeye ndiye aliyetuonyesha na kumtambulisha Baba bila makosa! 


Naamini imeeleweka! 


Samuel Peter 05/01/2021

No comments:

Post a Comment