Tuesday 31 July 2018

MISINGI YA KUMPATA MKE/MUME SAHIHI

MISINGI YA KUMPATA MKE/MUME SAHIHI

BWANA YESU ASIFIWE SANA

Naomba leo tujifunze juu ya kumpata mtu sahihi katika maisha kwa wale wanaotamani sana kuwa na mahusiano bora katika ndoa zao.

UPOFU
Katika kumtazama mtu sahihi katika maisha yako unaweza ukatazama kwa macho ya kawaida ukachanganya na maoni ya watu wengine na wote wakakupongeza lakini kumbe umepigwa upofu.
Ili usiendelee kumtafuta gizani katika hali ya upofu ni lazima upate nuru katika macho yako ambayo hiyo nuru hutaipata kwa marafiki, ndugu wala wazazi wako bali utaipata kupitia neno la Mungu tu na ukijifanya mjuaji utakuja kujuzwa uliyopaswa kuyajuwa kabla hujachukua maamuzi yako na kumuoa au kuolewa naye.

2WAKORINTHO 4:3-4
Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;

ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

******************
Kama hujamtazama kwa kutumia neno la Mungu basi hesabu maumivu kabisa katika hiyo ndoa.
Kama injili ilisitirika kwako ukaiweka pembeni basi ujue ulipotea njia katika hayo mahusiano.

mungu wa dunia hii ambaye ni shetani anapopofusha fikra zako basi hutataka kabisa kumtazama yeye kupitia neno la Mungu kwamba linasemaje juu yake.
Watu wengi wanapenda kuangalia kwa akili zao wenyewe na hata wanapoona kabisa mambo siyo mazuri katika hayo mahusiano huwa wanajifanya hawaoni kwaajili ya kulinda maslahi yao binafsi waliyoyaona kwa huyo mtu pengine ni muonekano, fedha au mali alizo nazo.

METHALI 31:30
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili;Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.

****************
Hapa ndiko penye upofu mwingine hasa kwa wanaume wengi.
Upendeleo unaozungumziwa hapa ni ile hali ya kufanya kitu kwa mtu asiyestahili.

Upendeleo ni Neema.

Kwa mfano sisi tulio ndani ya Kristo tumeokolewa kwa neema na siyo kwamba tulistahili sana.
Hivyo ulivyo wewe ni kwa neema tu siyo kwamba unastahili sana au una point yoyote ya kumwambia Mungu kwamba ulistahili uwe hivyo.
Sasa usije ukampenda msichana kwa upendeleo yani unamuona kabisa hana sifa za kuitwa mke halafu wewe ukamfanya kuwa mke.
Huo ni upendeleo lakini biblia inakuambia kwamba hudanganya.

Uzuri ni ubaliti lakini haimaanishi usiwe na mwanamke mzuri anaekupendeza, ila tu ule uzuri wake kisiwe ni kigezo cha yeye kuwa mke wako.
Nasisitiza kwamba ule uzuri wake kisije kikawa  ndicho kigezo cha wewe kumfanya kuwa mke.

Ubatili ni jambo lisilodumu na la kupita.
Uzuri huwa unapita maana hii miili yetu inaharibika lakini roho haipiti wala haizeeki ndiyo maana neno linasema kwamba mwanamke amchaye Bwana ndiye atakayesifiwa.
Kama ukipambana na uzuri na kuushikilia ujue ni lazima wewe utashindwa maana uzuri utakushinda na utakuacha na kuufuata uzee.

Kama mwanamke amchaye Bwana ndiye atakayesifiwa wewe unaelewa nini unapomuona mchumba wako anakuwa kipingamizi katika mambo yanayomhusu Mungu?

JE HUYO MWANAMKE ATASIFIWA NA NANI?

METHALI 3:4-5
Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri,Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

*****************
Ili uheshimike na upate kibali kwa Mungu na kwa wanadamu ni lazima umtumaini Bwana.

Kama unasemwa na watu na hujapata kibali kwao usije ukajitia kiburi kwa kusema eti mimi simsikilizi mwanadamu na wakati huo hata Mungu hujamsikiliza wala humsikilizi pia.

MANENO YA MWANADAMU YANAKUWA HAYANA NGUVU ENDAPO YANAPINGANA NA MANENO YA MUNGU.

Mshitaki wetu sisi ni shetani naye anazunguka zunguka akitafuta mtu ammeze.
Wale unaowaona ni watu wasio na akili na waovu ndiyo hao hao wanaokuambia ukweli juu ya mwenza wako.

Sasa hupaswi kweli kusikiliza maneno ya watu lakini unapaswa kuangalia neno la Mungu je, linaongea nini juu ya haya nayoambiwa na hawa wanadamu.
Uzuri ni kwamba hakuna kitu chochote hapa duniani ambacho biblia haijazungumzia.

Ikiwa wanaongea maneno yao wenyewe yasiyo na kibali mbele za Mungu unapaswa kuyapuuza.
Lakini ikiwa wanayoyaongea yana maana na yanakufundisha ni kwanini usiyasikilize?

AMOSI 3:3
Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?

*****************
Kwanza unatakiwa ujue ndoa ni agano baina ya watu wawili walio amua kuingia katika safari moja yenye lengo moja katika maisha.

Ni lazima kwanza mpatane mnachotaka kukifanya.
Lakini kama unaona mwenzako kuna mambo huwa mnabishana kila siku na hataki kabisa mpatane huyo anafaa kuingia kwenye ndoa?
Neno la Mungu linakuambia hamwezi kwenda pamoja.

Kila siku mnapatana kuwa waaminifu na wasikivu lakini mwenzako yeye anavunja yale mapatano kila wakati na unaendelea kung'ang'ana naye, unataka Mungu akuonyesheje kwamba huyu mtu hampatani?

Simaanishi kwamba hakuna madhaifu lakini unatakiwa utumie uwezo wa akili yako kuangalia wastani wa mambo mengi mnayopatana je huwa mapatano yanadumu au mengi huwa yanakiukwa?

Huyo ni mchumba tu na mnasuluhisha mambo kila siku jiulize mkifunga ndoa itakuwaje?
Mungu wetu ni mwaminifu maana anasema huwezi ukamwomba mkate akakupa jiwe.
Huwa anakuonyesha mapema lakini unajifanya huoni kwaajili ya tageti zako kwa yule mtu.

YOELI 2:28
Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;

****************
Hili neno ni kweli kabisa na nilitaka tu tuone hapa alikosema vijana wenu wataona maono.

Ni kweli kabisa vijana tunaona maono na hata wewe huwa unaona maono lakini unapuuza.

Unapokuwa mtu uliye makini huwa unaonyeshwa mapema kabisa ila unajifanya huoni.

Unaweza ukamwona msichana kwa mara ya kwanza kabisa kavaa suruali na ukavutiwa nae.
Lakini hapohapo mawazo yanakuja haraka kwamba.

KUMB 22:5
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.

*******************

Hapo sasa unamuona ni mzuri lakini pia neno la Mungu limeshamtafsiri kwamba yeye ni chukizo kwake.
Unataka uone maono gani tena?

HAYA NDIYO MAONO

Unapomuona Mwanaume/Msichana kwa mara ya kwanza kabisa halafu moyoni mwako ukamtoa kasoro ya tabia kulingana na muonekano wake, ujue ile ile tafsiri ya kwanza kabisa moyoni mwako hayo ndiyo maono yako lakini ikiwa inatafsiriwa na neno la Mungu.
Ikitokea ukajiliwaza kwa sababu zako binafsi basi ujue hayo ni mawazo ya shetani na unapingana na Mungu.

Yanaweza yakaja mawazo ya kwanza kabisa ukawaza moyoni mwako (HUYU NIMEVUTIWA NAYE LAKINI HAWA WASICHANA WANAOUZA BAR HUWA NI MALAYA TU)

Hiyo ni sauti ya Mungu kabisa lakini utakapoendelea kumtafakari kwa kumtazama utaingiza upendeleo na shetani naye anakuja kutia maneno yake ya kukuaminisha kwamba ni mtu sahihi.

Nakuhakikishia endapo utakuwa na mahusiano na yule msichana na ikatokea mkaja kuachana basi mtakuja kuachana kwasababu ileile uliyoiona kwake mwanzo kabisa ambayo ni umalaya.
Utamlaumu nani?
Ndiyo unaanza kusema, yani huyu hata siku niliyomuona tu kwa mara ya kwanza nilijuwa ni malaya.
KWAHIYO??  Kama ulijuwa ni malaya tukusaidieje?

KUWA NA MTU SAHIHI UPATE MATOKEO SAHIHI.

AKILI

Umeshamuomba Mungu juu ya mke mwema/mume mwema na wewe sasa unatakiwa uanze kuwa mwema kwanza ili upate wa kufanana na wewe.
Usifikiri unaweza ukampata mwema ikiwa wewe ni mwovu.
Usitarajie kabisa uwe waruwaru halafu umpate mtulivu.
Ndege wanaofanana huruka pamoja.
Wewe kama ni kupiga picha unajibinua binua kwenye mitandao yote ya kijamii ujue utakutana na mjinga mwezako huko huko mkavurugane.

Hili jambo la kutumia akili limekuwa ni changamoto pia.
Mwanaume/msichana anaweza akawa mcha Mungu na amesimama vyema kabisa kiroho lakini hatumii akili na kila kitu yeye ni maombi.
Hili nalo ni tatizo kumpenda Mungu kwa roho tu bila akili.

MATHAYO 22:37
Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.

*****************
Unapopenda kitu chochote ni lazima vitu vyote hivi vitumike ili ule upendo uwe salama kwako na ndiyo maana hata Mungu anasisitiza kwamba usipotumia akili yako yote hutaweza kumpenda.

Kupenda kwa akili siyo kosa maana hizo akili ni mali ya Mungu pia.
Kupenda kwa moyo ni ile hali ya kupenda na kutokuona hata udhaifu, kupenda bila kuwa makini, yani hujali hata watu watakuonaje bali unachotaka wewe ni kutimiza haja ya moyo wako.
Sasa hapo unakuwa umezama vilindini na kuzika fikra zako zote.

Hutumii akili hata kama kuna mambo unafanyiwa  ya kijinga lakini huoni maana fikra zako zimepofushwa na hata anafika hatua ya kukutenganisha na Mungu lakini unaendelea kuamini kwamba katoka kwa Mungu.

Yani hujali wala hutumii akili kuangalia je, huyu mtu ataweza kusimama kama mwanaume na kuwa kiongozi wa familia?
Huoni kama hajishughulishi na hatanui akili zake ili kuwa na maendeleo bali unachoangalia wewe ni Bwana asifiwe.
Utaenda kula kwa Bwana asifiwe?
Paulo mwenyewe alijuwa kuna Bwana asifiwe lakini akawaambia ikiwa mtu hataki kufanya kazi basi asile chakula.
Na pia Mungu anasema atabariki kazi za mikono yako.
Kama hufanyi kazi atakubarikije?

Uko na mwanamke kila muda sababu za kutaka fedha kwako haziishi lakini hutumii akili kujuwa kwamba huyo ni hasara katika maisha yako.
Je huyu kweli anafaa kuwa mke na maisha yakaenda sawa?

Yani muda mwingine mwanamke anakufanyia jambo la ajabu sana lakini akija amekuvalia kimini basi kesi inaisha.
Wewe hutumii akili lakini yeye anatumia akili na ndiyo maana akajuwa hiyo ndiyo dawa yako na kweli akafanikiwa.

USIPOTUMIA AKILI ZIKAONGOZA MAAMUZI NA UDHAIFU WA MOYO NA MWILI WAKO DUNIA ITAKUNYOOSHA TU.

Moyo unaweza ukakuambia siwezi kuwa mbali na huyu lakini akili ikakuambia huyu siyo mtu salama kwako.

Mwili na hisia vinaweza kukuambia kwamba haiwezekani kabisa kuwa mbali na huyo mtu lakini akili zinakuambia siyo kuwa naye mbali tu bali hafai kabisa hata kuongea naye kwenye simu.

Ni mzuri kweli ameushika moyo wako na hisia zako zote ni juu yake wala huoni mwingine.
Lakini ana kiburi cha maana, siyo mwelewa, dunia imemkamata sawasawa, hana heshima, hamsikilizani, wala hayupo makini, mgomvi, hafundishiki wala ukimuonya haonyeki.

1PETRO 3:7
Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.

*****************
Mungu anavyosema ukae nae kwaakili hamaanishi kwamba uache kumtegemea.
Kuna vitu vinakuwa nje ya uwezo wa akili zako hivyo ndivyo huwa Mungu huja hujitwalia utukufu.
Lakini kuna vingine unatakiwa utumie akili.
Siyo unasema kila kitu ni maombi tu bali ni maombi huku ukitumia akili kutoka kwenye hizo shida halafu Mungu ataiwezesha akili yako kuwaza hadi kufikia lengo.

Wapo watu hawajaokoka wala hawana mpango na Mungu lakini kwa kutumia akili za kawaida tu ambazo hata hazitokani na Mungu wamefanikiwa.
Sasa wewe uliye na Mungu ukitumia na akili za KIUNGU si utakuwa zaidi?

Kwani Mungu alishindwa nini kusema ukae na mke wako kiroho tu?
Akili Mungu anayotaka uitumie hapa ina kazi gani?

Usikae tu na mwenza wako halafu ukajipa moyo tu kwamba sisi tumeokoka nakuambia utalea hata watoto wa watu maana shetani yupo kuleta majaribu.
Unataka Mungu akuambie kwamba huu siyo muda wa mke wako kubeba ujauzito kama anakuletea ujauzito ambao hukulala nae siku za yeye kuweza kubeba huo ujauzito?

OGOPA DHAMBI, MTII MUNGU, TUMIA AKILI NA USIMTENDEE MWENZAKO JINSI USIVYOPENDA WEWE KUTENDEWA NAKUHAKIKISHIA UTAYAWEZA YOTE.

#Powered_By_Holly_Spirit

IN ENGLISH

METHOD FOR RECEIVING MARKET / MISS MEETING

JESUS ​​IS NOT ASKED

I pray today to learn about finding the right person in life for those who long to have the best relationships in their marriage.

PROFILE
In looking at the right person in your life you can look at the ordinary eyes and blend with the views of other people and all of them praising you but being blinded.
To keep on looking for darkness in a blind state you must have a light in your eyes that the light will not find by friends, relatives or parents but only through the Word of God and pretending to know what you should be aware of before making your decisions and getting married.

2 CORINTHIANS 4: 3-4
But if our gospel is frustrated, it is overlooked to those who are lost;

in whom the god of this world has blinded the minds of the unbelievers, not to shine on the light of the gospel of the glory of Christ, who is God's image.

******************
If you do not look at God's word then calculate the pain in the marriage.
If the gospel was reluctant to you and put it aside, then know that you lost the way in these relationships.

The god of this world, who is Satan, is blinding your thinking, so you will never want to see him through the Word of God what it says about him.
Many people like to look at their own ideas and even when they see things uncomfortable in these relationships they tend to do not see the aim of protecting their personal interests that they have seen from the person who is perhaps the appearance, money or possessions they possess.

ACTS 31:30
Pride deceives, and beauty is vanity: but the woman that feareth the LORD shall be accounted for.

****************
Here is another blindness for most men.
The privilege mentioned here is the state of doing something to the unworthy person.

Privilege is Grace.

For example, we who are in Christ are saved by grace and not necessarily deserved.
So what you are by grace is not just that you deserve so much or you have any point to tell God that you deserve to be so.
Now do not love the girl for the privilege you see her absolutely does not have the reputation of being a wife then you make her a wife.
That is a privilege but the Bible tells you that you are deceiving.

Beauty is betrayal but it does not mean you do not have a beautiful woman, but her beauty is not a criterion for her to be your wife.
I insist that its beauty does not matter if it is a criterion for you to make her a wife.

Violence is an indefinitely lasting thing.
Beauty is passing through because our bodies are corrupted but the soul is not infinite and it is not impossible because the word says that the woman who hates the Lord is the one who will be told.
If you struggle with beauty and hold fast to yourself you must fail and mean beauty will win you and you will leave you and follow it old.

If a woman hates the Lord is the one who will be told you understand when you see your boyfriend becoming an obstacle to things about God?

WHO IS THE WOMAN DESIGNED?

METHOD 3: 4-5
So you will gain the favor and good sense, the forehead of God and the human being.

Trust in the LORD with all your heart, and do not lean on your own mind;

*****************
In order to honor and gain favor with God and for humankind you must trust the Lord.

If you are spoken by people and you have not received the approval of them lest you be proud of saying that I do not listen to man at that time even though God listens to him or hears it too.

MANUAL INVESTMENTS CAN NOT HAVE A FOLLOWING LIFE THAT IS LIKE GOD'S WORDS.

Our accuser we are Satan and he circulates around looking for someone to accuse him.
Those you see are unwise and wicked people are the ones who tell you the truth about your partner.

Now you should not listen to the words of men but you should look at the word of God what does he say about what these are told to these human beings.
The beauty is that there is nothing here on earth that the Bible has not spoken about.

If they speak their own unfamiliar words before God you should ignore it.
But if they speak it meaningful and what they teach you why do not you listen?

Amos 3: 3
I am Can two walk together, unless they have agreed?

*****************
First you should know marriage is a covenant between two people who have chosen to enter one single-day journey in life.

You must first get along with what you want to do.
But if you see your partner there are things you're arguing each day and do not really want the girlfriend to get married?
The Word of God tells you you can not go together.

Everyday you are honest and caring but your partner breaks the treaty every time and keeps looking at him, wanting God to show you that this person does not fit?

I do not mean that there is no weakness but you should use your mental ability to look at the average amount of things you agree on whether the contract lasts or most is being violated?

That's just a boyfriend and you're solving things every day ask yourself how to get married?
Our God is faithful because He says you can not ask for bread and give you a stone.
They are showing you in advance but you are pretending not to fit for your traits to that person.

Joel 2:28
And it shall be, after that, that I will pour out my spirit upon all flesh; and your sons, and your wives, shall prophesy, and your old men shall dream dreams, and your young men shall see visions;

****************
This word is quite true and I just wanted to see here that he said your teenagers would see a vision.

It's really young people we see visions and even you see visions but you ignore.

When you are a careful person you are shown in advance even if you make yourself unfamiliar.

You can see the girl for the first time in dressing pants and attracted to her.
But then the ideas come quickly that.

REVELATION 22: 5
The woman shall not put on the apparel that is upon a man, neither shall the man put on the apparel of a woman; for every one that doeth these things is an abomination unto the LORD thy God.

*******************

Now you see him good but also the word of God has translated him to be a disgusting thing to him.
What vision do you want to see?

THERE ARE WORDS

When you first see the man / girl then in the heart you give him the flaw of character according to his appearance, know the same original interpretation in your heart that is your vision but if it is translated by the word of God.
If you happen to fall for your own reasons then know that it is Satan's thinking and contradicts God.

They may come up with the first ideas that you think in your heart (OUR HEART WITHOUT THE BEST OF THE FOLLOWING BABY THERE ARE OUR LIFE)

That is the voice of God completely but when you keep meditating on it you will get a favorable influence with the devil and he comes to put his words to convince you that he is the right person.

I assure you that if you have a relationship with the girl and it comes to abandoning you then you will have to leave because of what you saw at the very beginning that is a malaria.
Whom will you blame?
Yes you begin to say, who the only day I saw him for the first time I knew it was a shirt.
SO?? If you knew how coat would help you?

THERE IS NO HUMAN RELATIONSHIP WITH EXPERIENCE.

NOT

You have asked God about a good husband / husband and you now have to start to be good first to get the same as you.
Do not think you can find him good if you're bad.
Do not expect to be truly wise and then get calm.
Birds that match are moving together.
You like the photography that elevates the binus on all social networks knowing you will meet a friendly fool there in the autumn.

This sense of mind has also been a challenge.
A man / woman can be a hypocrite and stands up spiritually but does not use the mind and everything he is praying for.
This is a problem with loving God only with the spirit without understanding.

MATTHEW 22:37
And he said unto him, Thou shalt love the Lord thy God with all thy heart, and with all thy soul, and with all thy mind.

*****************
When you love anything, all these things must be used so that your love will be safe for you and that's why God insists that you will never be able to love it.

Mind of mind is not a mistake that mind is God's property too.
Heartfelt love is a tendency to love and even to lose sight of weaknesses, to love without paying attention, who care about how people will treat you but what you want is to fulfill the need for your heart.
Now you're drowning in the bottom and bury all your thoughts.

It does not use intelligence even though there are things that are stupid and you do not see why your thoughts are blinded and even come to the point of separating you from God but you still believe that it comes from God.

Who cares or does not use the mind to see whether this person will be able to stand as a man and be a family leader?
You do not think you're not busy and do not want his mind to be successful but what you look for is the Lord to be saved.
Will you go to the Lord for food?
Paul himself knew that there was no Lord to be told but he told them if anyone would not work and then not eat food.
And also God says he will bless the work of your hands.
If you do not work, how will he bless you?

You always have a woman who wants to spend money with you but do not use it to realize that it's a loss in your life.
Does this really fit as a wife and life goes well?

What else does a woman do for you a wonderful thing but she comes dressed in hell then the case ends.
You do not use intelligence but he uses intelligence and that's why he knew that's your medicine and he really did.

NOT USE THE EFFECTS OF THE HEALTH AND LIFE OF YOUR LIFE AND YOUR HEALTH PRODUCTS.

The heart can tell you I can not be away from this but the mind told you this is not a safe person for you.

Body and emotions can tell you that it is impossible to be far away from the person but the mind tells you not to be away from him but not even to talk to him on the phone.

It's really nice to touch your heart and all your emotions are on it and you do not see another.
But he has a great pride, not in a sense, the world has caught him in the same way, has no respect, no attention, no attention, no strife, no discipline or no warning.

1 Peter 3: 7
Likewise, ye husbands, abide with your wives in mind; and to give her the honorable wife, as a weaker vessel; and as joint heirs of the grace of life, that your supplication may not be hindered.

*****************
What God says to stay with Him does not mean that you have to rely on Him.
There are things that are out of the power of your mind so God comes and gives you glory.
But there's another you need to use the mind.
Not only do you say everything is an application but it is an application with insight from those problems and then God will allow your mind to appeal to the goal.

There are people who are not saved and have no plan with God but with the only common sense that they are not even from God they have succeeded.
Now you with God using the mind of GOD will not be more?

For what did God fail to say to live with your wife only spiritually?
What kind of mind does God want you to use here?

Do not just stay with your partner and then just give us the impression that we have saved and told you to nurture even the children of men that Satan is presenting temptations.
Do you want God to tell you that this is not your time to bear pregnancy if it causes you to have sex that you do not sleep on for days to carry that pregnancy?

OGOPA DHAMBI, OTHERS GOD, DETERMINATE YOURSELF AND DO NOT APPLY YOUR EFFECTS THAT YOU NEED TO BELIEVE AND IMPLEMENTATE YOU CAN ALL.

#Powered_By_Holly_Spirit

No comments:

Post a Comment