Tuesday 31 July 2018

MISINGI MUNGU ALIYOIWEKA KATIKA KUJIBU MAOMBI YETU.

BWANA YESU ASIFIWE

MISINGI MUNGU ALIYOIWEKA KATIKA KUJIBU MAOMBI YETU.

Ni utaratibu ambao Mungu ameuweka ili kila mmoja atakayeufuata maombi yake yajibiwe na anatamani sana sisi watoto wake tuujue ili kuonewa na Yule mwovu kukimbie kati yetu.

Hakuna njia nyingine yoyote ya MTU kujibiwa maombi yake endapo hatafuata misingi hii.
Ndiyo maana unatakiwa uijue maana usipoijuwa hakuna namna yoyote ya Mungu kukuhurumia na kukujibu eti kisa hujui.

Maana kusudi la Mungu kukuumba ni ili umjue na kumpenda kisha umtumikie.

Sifa na utukufu ni kwa Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo ambaye muda wote anatuwazia mema tu.
Kwa uwezo wa Roho wake Mtakatifu Leo amekusudia kutufunulia tena siri za mbinguni kwa wema wake tu ili tupate kuzijuwa mbinu za kumshinda yule baba wa uongo.

Lengo la somo hili ni kumwezesha kila mmoja kumwendea Mungu na kutokuwa na Shaka kwamba hajasikiwa au kujibiwa.
BWANA YESU ASIFIWE SANA.

Neno la msingi katika mafundisho yetu ni

MARKO 16:17A
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;

******************

Naposema MARKO sura ya 16 mstari wa 17A inamaanisha kwamba unapoona katika andiko mwisho wa mstari kunakuwa na alama hii ; inamaanisha huo mstari unajitegemea.

Sasa Leo tutauchambua huo mstari kwa undani zaidi.

MARKO 16:17A
Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio;

*****************

Ishara ni muujiza wa kiungu unaotokea kwa mwombaji aliyeamua kumwelekea Mungu.
Sasa Mungu anasema kwamba ili hizo ishara zije kwako ni lazima kwanza uliamini neno lake kwamba linamaanisha kwamba ni kweli kabisa kile linachokiongelea.

Je, ni kweli huwa Mungu anakusikiliza kila wakati unapokuwa unaomba?

Mungu bado anafanya Kazi mpaka sasa hivi?

MAJIBU
Mungu alishamaliza Kazi tangu mwanzo na alishauweka utaratibu au misingi kamili ambayo inamuonyesha kwamba bado anajishughulisha lakini ukweli ni kwamba yeye kwa sasa ameketi katika kiti chake cha enzi huku misingi yake ikifanya Kazi.

Yani ni kama wewe umefanya Kazi ukiwa kijana ukajiwekea miradi mbalimbali ambayo itakusaidia wewe utakapokuwa mzee uwe umetulia tu nyumbani lakini unaingiza fedha kila siku.
Huo uwezo wa kujiingizia kipato huku hujishughulishi ni kutokana na misingi uliyoiweka tangu awali.

MWANZO 1:27-28
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

****************

Mungu alikusudia kabisa sisi wateule tuwe kama yeye lakini tumeshindwa kuzitumia nafasi zetu.
Ndiyo maana akatuumba kwa mfano wake na kila kilicho chake akakiweka ndani yetu ili tu tuvitumie na kufikia viwango vyovyote tunavyotaka na anavyotaka yeye pia.
Mungu siyo mwoga, siyo mwongo, hashindwi, hasemi uongo, na akitamka tu neno inakuwa.

Mungu ametuambia tuzaane na kuongezeka, zaidi ya yote pia tuitiishe nchi na kila kiumbe.
Mungu asingeweza kutuagiza kufanya mambo yote hayo ikiwa hajatuwekea vitendea Kazi.

MWANZO 2:2
Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

******************

Mungu alipomaliza Kazi yake yote hapo mwanzo, hakuna mahali popote ambapo biblia inatuambia kuwa alirudi tena kufanya kazi.
Aliacha kazi yake yote aliyoifanya ili iendelee kwa namna alivyoiwekea mfumo na msingi imara.

Mungu alivyoiumba dunia na vyote vilivyomo alimaliza kazi yote na hakuja kurekebisha tena kitu chochote.

Mungu huwa hawazi kila siku na wala hapati akili mpya au eti akili yake iongezeke.
Alivyowaza mara moja tu paaaaaaaaaaaaaaaaaaa aliwaza kuanzia MWANZO mpaka UFUNUO.

Kwa sasa NENO lake ndilo linalofanya kazi maana NENO linaongea, neno liko hai na neno ndilo mrithi wa yote.

WAEBRANIA 1:1-2
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

*****************
Mtendaji wa kazi kwa sasa ni Neno ambaye ni YESU KRISTO na katika hilo neno ndiko tunakotimiziwa ahadi zote zilizoko ndani yake.

Ndiyo maana unapoomba hata uombeje kama hujatumia neno ili hilo neno likusikie na lithihirike kwako ujue hakuna jambo jipya litakalotokea kwako.

MATHAYO 18:19-20
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.

****************

Yesu anasema wawili watakapopatana duniani katika jambo lolote Baba atawafanyia.
Anatoa na sababu kwamba Baba atawafanyia kwakuwa yeye yuko hapo.
Mungu anajibu kupitia neno lake ambalo ni YESU KRISTO.

Pia anasema anakuja kuangalia neno lake ili alitimize.

ISAYA 55:10-11
Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;

Ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

******************

Mungu analifananisha neno lake na mvua na anasema litatimiza.
Anasema litatimiza kwasababu utakapofuata maelekezo sahihi katika kuomba kwako basi lile neno litatimiza na siyo kwamba Mungu atakusikiliza tena na kukutendea.

Yani lile neno linakutambua wewe na lipo pale kwaajili yako ili litimize mapenzi ya Mungu kama ni kukubariki likubariki au kama ni kukulinda likulinde.

Neno ni kama mvua maana mvua inaponyesha huwa kuna MTU inamfaidisha na kuna MTU haimfaidishi.
Inamfaidisha aliyepanda mbegu lakini kama hujapanda mbegu hutakuwa na faida na hiyo mvua.

Kwamfano neno lipo kabisa linasema nitakuponya na ni neno la Mungu la kweli na hakika.
Sasa wewe ni mgonjwa na unapomwomba Mungu akuponye hujataja hilo neno ili likuponye
Yani hapo hilo neno lilipo hujapagusa wala hujalitaja ili lije likuponye.
Hapo hutapona maana lile neno halitakuja.

Ili neno litimize linachosema ni mpaka uwe na uhitaji na hilo neno.

POINT
UKIOMBA MOJA KWA MOJA KWA MUNGU BILA KUTUMIA NENO LAKE HATAKUSIKIA.
WALA MUNGU HAJAWEKA UWEZEKANO WA KUKUSIKIA BILA KUTUMIA NENO LAKE.
MAANA ALISHAIMALIZA KAZI YAKE PALE MWANZO NA KILA KITU AMEACHIA NENO LAKE LITUHUDUMIE.
YEYE HAFANYI TENA KAZI YOYOTE YUKO KWENYE KITI CHAKE CHA ENZI AMETULIA BWANA WA MAJESHI.

Ukiwa na neno ndani yako neno litakutambua na kutimiza mapenzi ya Mungu kwako katika Jambo lolote unalohitaji.

Hakuna uwezekano wa Mungu kukusikiliza ikiwa umeomba vibaya bila kufuata neno lake.

MFANO
Kama unaona mifumo wanayoitumia wenye mitandao ya mawasiliano ya simu za mkononi.

Unapopiga namba ya huduma kwa wateja huwa ukifuata maelekezo unayoambiwa utajikuta umeshajibiwa shida yako pasipo kuongea na mtoa huduma.
Lakini ukikosea tu simu inakatika mawasiliano wala hutapata msaada.
Huwa unapopiga ile namba hakuna MTU anaekusikiliza Bali ni mfumo umewekwa hivyo ili wateja watakapofuata maelekezo watatuliwe shida zao.

Ndiyo hivyohivyo Mungu ameweka mfumo katika neno lake inakubidi ufuate misingi ya kuomba.

Lile neno liko kwaajili yako na linakusubiri wewe gombel uliguse ili likutendee mapenzi ya Mungu.
Nachosisitiza tu kwa sasa ni wewe kujuwa kwamba neno la Mungu ndilo linatenda sasa mpaka atakapobatilisha utatu mtakatifu.

1WAKORINTHO 15:24-28
Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.

Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.

Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti.

Kwa kuwa, Alivitiisha vitu vyote chini ya miguu yake. Lakini atakaposema, Vyote vimetiishwa, ni dhahiri ya kuwa yeye aliyemtiishia vitu vyote hayumo.

Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.

***************

Tunaona kabisa kwa andiko hili kwamba Yesu Kristo ndiye mtendaji wa yote katika ahadi iliyo katika neno kwani mamlaka yote mbinguni na duniani  amepewa yeye.
Hakuna kinachofanyika bila utatu mtakatifu na mpaka baada ya yote ndipo utabatilishwa.

Ili neno la Mungu litimize linachosema kwako sasa unapaswa uliamini na ndiyo maana katika neno letu la msingi linasema kwamba ishara zitafuatana na hao waaminio.

Ili uamini ni mpaka uwe na imani ambapo biblia inatuambia

WAEBRANIA 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.

***************

Neno linaongea kitu ambacho hakionekani katika macho ya kawaida na haijalishi hukioni Bali unatakiwa ukiamini tu.
Utakapoamini ndipo ishara itakuja na kuiona.

Hutakiwi kuhitaji kuona kwanza Bali unaposikia tu neno unatakiwa kuliamini moja kwa moja ndipo ishara itakuja na kupokea haki yako iliyobebwa na hilo neno.

WARUMI 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

****************

Mungu anasema

WAEBRANIA 10:38
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.

HABAKUKI 2:4
Tazama, roho yake hujivuna, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa imani yake.

******************

Ili haki yako iliyobebwa ndani ya neno ionekane kwako kwanza ni lazima uamini kwa kusikia lile neno ndipo ishara yake ikufuate wewe uaminiye.

Wakati unaomba bila kufuata utaratibu wa Mungu huwa unajiweka katika nafasi ya kutokupata msaada wowote.
Huwa Mungu anatamani akusaidie lakini tatizo alishaweka mrithi ambaye ni Yesu Kristo (NENO) na hawezi kuingilia tena.

WAEBRANIA 1:1-2
Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi,

mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

*****************
Kwa misingi hii tunaona kabisa kwamba Mungu hafanyi tena Kazi kwa sasa Bali amemweka mwana kuwa mrithi, mwana ambaye ni Yesu na Yesu ambaye ni Neno.

Hivyo utakapoliamini lile neno kwa kulisikia ndipo ishara na ahadi zilizopo katika hilo neno zitakapokufuata wewe.
Vinginevyo utaomba sana lakini hutapata msaada wowote.
Badala yake atakuwa anasikitika tu kwa wewe kushindwa kuyajuwa maarifa na anabaki akisema.
WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA.

NAKUSHUKURU SANA ROHO MTAKATIFU KWA KUACHILIA TENA UFAHAMU HUU.
SIFA NA UTUKUFU NI KWAKO ROHO WA BWANA.

MUNGU AKUBARIKI SANA KWA JINA LA YESU KRISTO.

#Powered_By_Holly_Spirt

IN ENGLISH

THE LORD JESUS ​​IS NOT DONE

GOD'S CHILDREN MAY BE REQUIRED IN OUR NEXT FOR OUR NEXT.

It is the order that God has set for each one to follow his prayer and to desire his children to know it to be seen by the Evil One to flee among us.

There is no other MT solution to respond to its application if it does not follow these principles.
That's why you should know what it means when you do not know it's not God's way to sympathize with you and tell you the story you do not know.

For the purpose of God is to make you know and love Him and then to serve Him.

Glory and glory are to the God of our Lord Jesus Christ who always imparts us to good.
By the power of His Holy Spirit, He has purposed to reveal to us the mysteries of heaven for His goodness only to understand the ways of overcoming the false father.

The purpose of this lesson is to enable each other to come to God and not to have any doubt that he is not impressed or answered.
JESUS ​​IS NOT ASKED.

The key word in our teaching is

Mark 16: 17A
And these signs shall be with those who believe;

******************

I read MARKO chapter 16 verse 17A means that when you see in the text the end of the verse contains this mark; means that line is independent.

Today we will analyze that verse in more detail.

Mark 16: 17A
And these signs shall be with those who believe;

*****************

The sign is a divine miracle that occurs to the requester who has decided to approach God.
Now God says that in order for these signs to come to you you must first believe his word that means that is exactly what it is talking about.

Is it really God that hears you every time you pray?

Does God still work until now?

ANSWERS
God has completed the work from the beginning and has set up a perfect order or basis that shows him that he still cares for himself but the fact is that he is now sitting on his throne with its foundations working.

What if you've worked as an adolescent and set up a variety of projects that will help you when you are old enough to get home at home but earn money every day.
The ability to earn income while engaging in it is based on the principles you set before.

ACTS 1: 27-28
God created man in His image, in the image of God created, man and woman created them.

And God blessed them, and God said unto them, Be fruitful, and multiply, and replenish the land, and subdue it; control the fish of the sea, and every living creature that moves on the earth.

****************

God wanted us to be like him but we failed to use our positions.
That is why He created us in His image and everything He has put in us so that we can apply it and meet whatever we want and what He wants us to do.
God is not a coward, it's not a lie, a failure, does not lie, and just say the word becomes.

God has told us to grow together and grow, and above all, let us satisfy the earth and every creature.
God could not have commanded us to do all these things if he did not let us work.

ACTS 2: 2
And on the seventh day God finished all his work which he had done; He stayed on the seventh day and stopped doing all his work he had done.

******************

When God finished His work in the beginning, no place where the Bible tells us that he returned to work.
He left all his work to continue in the way he set up with a solid foundation.

God created the universe and everything in it he finished all work and did not come to remedy any other thing.

God does not know everyday and he does not have a new mind or does his mind grow.
He once thought of himself at the point of view from the ONLY to the OPEN.

At present his word is working because NOW speaks, the word is alive and the word is the successor of all.

SECTION 1: 1-2
God, who spoke long ago with our fathers in the many parts and in many ways,

The end of these days has spoken to us in the Son, who has made him the heir of all, and to him who made the world.

*****************
The workpiece is now the Word that is JESUS ​​CHRIST and in that word we are fulfilling all the promises contained in it.

That's why you do not use the word so that the word will hear and stick to you, you know that no new thing will happen to you.

MATTHEW 18: 19-20
Again I say to you, that if you agree on earth in anything, whatever they ask, it will be done to them of my Father which is in heaven.

For where there are three gathered together in my name, and I am in the midst of them.

****************

Jesus says two will be united on earth in whatever the Father will do for them.
He gives the reason that the Father will do for them because he is there.
God responds through His word which is JESUS ​​CHRIST.

He also says he comes to look at his word to fulfill it.

ISAIAH 55: 10-11
For as the rain cometh down, and the snow from heaven, and cometh not thither; but it that eateth bread, and bringeth forth it, and giveth it to the man that soweth seed;

So my word, that goes out of my mouth; it will not return to me but it will accomplish my will, and it will succeed in the things I sent.

******************

God likens his word to rain and says it will accomplish.
He says it will be fulfilled because you follow the correct instructions in your request then the word will be fulfilled and not that God will hear you again and do it.

What the word recognizes you and is there for your subscription to fulfill God's will to bless you or to keep you from guarding you.

The word is like rain because rain suggests that there is a person who helps and there is no one who does not benefit.
It helps the plant to plant but if you do not plant the seed it will be beneficial and it will rain.

For example, the word exists and I will heal you and it is the word of the true God and sure.
Now you are sick and when you pray for God to heal you say that word to heal you
Where is the word there is no comment and no mention of it to come in.
There you will not feel that the word will not come.

For the word to fulfill what it says is until you need it with that word.

POINT
ASKING ONLY TO GOD DO NOT USE HIS NAME HAS NOT HAPPENED.
BEFORE GOD CAN NOT HAVE ETERNITY OF HUMAN RELATIONSHIPS TO USE HIS NAME.
HUMAN RELIGION HAS NOT HAPPENED HIS BODY IN HUMANITY AND HAS HAPPENED HIS NAME AND HIS NAME.
HE DO NOT HAPPEN TO ALL WORKS THAT HAVE BEFORE THE TOOL OF THE ENVIRONMENT OF THE ENVIRONMENTAL LEADERSHIP.

Having a word within you the word will recognize and fulfill God's will for you in whatever you need.

It is not possible for God to listen to you if you have prayed incorrectly without following his word.

Image
If you see the system they use with mobile phones.

When you enter a customer service you follow the instructions you are told you will find yourself responding to your problem without communicating with the service provider.
But if you're just mistaken, the phone is in contact and you will not get help.
When you call the number nobody listens But it's a system that is set so that customers will follow the directions will be set up for their problems.

So God has set the system in his word you have to follow the basis for praying.

This word is for your subscriber and it expects you to embrace it so that it can do God's will.
The only thing you can do now is that the word of God is what it is doing right now until it brings about the trinity.

1 CORINTHIANS 15: 24-28
That is the end, when he gives God the Father his kingdom; when he brings about all rulership, and all authority, and power.

For he must possess it, even to put all his enemies under his feet.

The last enemy to be abused is death.

Because, He put all things under his feet. But when he says, All things are fulfilled, it is obvious that he has left us all things is not.

When all things are finished under him, then the Son himself will also be subjected to him who has put all things to death, that God may be all in all.

***************

We find out in this verse that Jesus Christ is the one who is the greatest of all in the promise in the Word since all authority in heaven and on earth has been given to him.
Nothing is done without a sacred trinity and until after all it will be changed.

For the word of God to fulfill what it says to you now you should believe it and that's why in our basic word it says that the sign will accompany those who believe.

To believe it is until you have faith where the Bible tells us

READING 11: 1
So faith is the surety of things hoped for, the clearness of things that are invisible.

***************

The Word speaks something that does not appear in normal eyes and no matter what you see Bali you just have to believe it.
When you believe and the sign will come and see it.

You do not need to see first But when you hear the word you just have to believe it right and the sign will come and receive your right-handed word.

Romans 10:17
So faith, the source is to hear; and hearing comes by the word of Christ.

****************

God says

READING 10:38
But my righteous one will live by faith; And while he is still feeling, my soul is not happy with him.

Habakkuk 2: 4
Behold, his spirit is haughty, and is not upright in him; but the just will live by his faith.

******************

For your right to be enthroned in the word to appear first to you, you must believe in hearing the word and then sign it to follow you.

When you pray without following God's order, you keep yourself in the position of getting no help.
It is God's desire to help you but the problem lost the successor who is Jesus Christ (NOW) and can not intervene any more.

SECTION 1: 1-2
God, who spoke long ago with our fathers in the many parts and in many ways,

The end of these days has spoken to us in the Son, who has made him the heir of all, and to him who made the world.

*****************
On this basis we find that God is no longer active at present but has appointed his son to be an heir, who is Jesus and Jesus who is the Word.

So when you believe the word by hearing it is the signs and promises in the word that will follow you.
Otherwise you will pray very much but you will not get any help.
Instead, he will only be scared for you to know the facts and he remains to say it.
MY PEOPLE HAVE BENEFITED FOR NATURE INFORMATION.

REMEMBER AS THE HOLY SPIRIT BY EVERYTHING AND THINK YOU.
NOW AND GLORY IS THE LORD'S SPIRIT.

GOD IS NOT LIKE THE NAME OF JESUS ​​CHRIST.

#Powered_By_Holly_Spirt

No comments:

Post a Comment